Friday, 19 July 2019

'BADO RECORDS HAIWEZI MZIKI WANGU'


Msanii kutoka pwani ya Kenya,kaunti ya Kilifi anayekwenda kwa jina Timatsi ameiponda studio ya msanii mwenza Mr Bado iliyoko Watamu.Haya yametokea kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji Pascal Shanga na Mtu Bei kwenye kipindi cha Chachawiza ndani ya Bahari FM leo ijumaa tarehe 19.Timatsi amekiri kuwa studio ya msanii Mr Bado haina hadhi ya kumfanyia kazi zake kwa kuwa producer wa studio hiyo hajamakinika.


Ameongezea kwamba wakati alipokuwa chini ya himaya ya Bado Records, alikuwa akifanya tu mazoezi ya sauti yake ila hakuwa chini ya studio hiyo kikazi.Ikikumbukwa kwamba Timatsi ni msanii aliyekuwa miongoni mwa watu wa karibu wa Mr Bado na hata kuwa mwanachama wa KICOTA,kikundi kilichoanzishwa na Mr Bado.Kupitia mahojiano hayo,imebainika kuwa Mr Bado hakuwahi kufanya kazi zake kwenye studio yake ila kwenye studio za Crack Sound chini ya producer Jay Crack.Labda haya ndiyo yaliyopelekea kusambaratika kwa studio hiyo kwa kuwa kufikia sasa hakuna wasanii wanaofanya vizuri kutoka studio hiyo .Je ,studio hii imebaki kama mahali kwa kufanyia mazoezi kama alivyofunguka Timatsi ama alikuwa anaponda tu? Meza yetu ya habari inafuatilia habari hizi ili kubaini kama maneno ya Timatsi yana ukweli ama kuna mambo ya kibanafsi baina ya wawili hao.

2 comments:

  1. Kwa mtazamo wangu nadhani Timatsi hakupaswa kuongea maneno hayo kwa sababu amekulia hapo Bado Records, amekua akiimba Bado siku zote.
    Inanikumbusha wakati flani jamaa wa Kamua Leo alipohojiwa na kuulizwa kwamba remix ndio iliyomfikisha mbali alikejeli kwamba yeye mwenyewe mkali, matokeo kila Mtu anayafahamu.
    Tunatakiwa ku-appreciate pale tulipoanzia ata kama kulikua duni vipi.
    Ni mtazamo tu

    ReplyDelete
  2. Ni sawa.Mara nyingi mtu husahau pale alipokulia.Akijiona yuko mbele kushinda alipoanzia wengi hukataa alipotoka.!

    ReplyDelete