Thursday, 16 April 2020

WATAAMUA WENYEWE WAKIKUA / NAHISI VIPAJI VIPO



Mtoto wa nyoka siku zote hawezi kuwa mburukenge 😄. Na kweli hii inadhihirika katika hali halisi ya maisha ya sasa.Katika pekuzi zetu tulipata 411 kutoka mtaa anakotoka rapa anayeendelea kufanya vizuri katika tasnia ya mziki wa kizazi kipya kutoka pwani ya Kenya, Kilifi County tukimzungumzia Fash P.Hivi ushawahi kujipa wakati na kufuatilia kazi zake?Kama bado sisi kama NUKTASABA tumefanya hilo kwa ajili yako.Fash P amefanya kazi nyingi zikiwemo zake binafsi na ambazo ameshirikisha na kushirikishwa na wasanii wengine.Zipo ngoma kadhaa ambazo pia amezifanya video.Tumegundua kwamba baadhi ya watu anaowatumia kwenye video zake ni watoto wake wa damu.

Tukianza kwa kumulika video ya DEAR SON ambayo kwenye video hiyo kuna mtoto anayeonekana akipewa mawaidha na mkubwa wake,kwa video akionekana kama babake.Anayecheza nafasi hiyo ya baba kwenye video hiyo vile vile ni msanii anayefahamika kama Dallas Me na huyo mtoto ndiye wa kwanza wa rapa huyo.Hivi majuzi wasanii wakali kutoka Watamu walishirikina na kufanya ngoma ya hamasisho kuhusiana na janga hili la Corona.Kwenye ngoma hiyo pia yumo Fash P.Kwenye video ya ngoma hiyo kuna watoto wanaoonekana wameshika mabango yenye jumbe tofauti tofauti.Miongoni mwa watoto hao kuna mtoto anayeonekana ameshika bango lenye maandishi "SANITIZE" ,hapo weka pause.Huyo ndiye ninja wa pili wa Faaaaaash 😄 sema upekuzi mzee baba!

Tulitaka pia kuthibitisha tetesi hizo na ikabidi kumtafuta msanii huyo kwa njia ya simu."Yes,hao wote ni damu yangu.Wanapenda sana mziki na niliona bora nianze kuwaonyesha njia pole pole.Mengine wataamua wenyewe wakikua ila nahisi vipaji vipo" hayo yalikuwa maneno yake Fash kabla ya kumaliza mahojiano yetu. Unaweza kutazama video hizo hapo chini.Usisahau pia kusubscribe.

DEAR SON - FASH P





2 comments:

  1. Ni jambo la busara kushirikisha familia, heko kwa Fash

    ReplyDelete