Tuesday, 23 July 2019

PLANET KENYA ASAHAU KUWA MCHEZA KWAO HUTUZWA!


Kwa kipindi cha mda mfupi sasa,tumeona wasanii wakisahahu wanakotoka kwa jinsi wanavyoyajibu maswali kwenye mahojiano ya moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.Baada ya kuangazia matamshi ya Timatsi kuhusiana na Bado Records,kwenye bench leo tunamzungumzia Planet Kenya.Siku ya Jumatatu tarehe 22 mwezi huu wa saba ,Planet akiwa kwenye mahojiano na Pascal Shanga na Mtu Bei ndani ya Bahari FM kipindi cha Chachawiza alinukuliwa akiwakejeli wasanii wa nyumbani ,Malindi."Wasanii wa Malindi ni wavivu pia ni wanafiki kwa kweli nilihama Malindi kwa sababu mziki wa Malindi uliniangusha.Nilifanya mziki kwa miaka kadhaa ila sikupata mafanikio"

Planet  alizidi kufunguka na kuelezea sababu zilizopelekea kusambaratika kwa kundi la Yakwetu "kuna wengi wanasema kundi letu lilisambaratika kwa sababu ya  mwanamke ila ni uongo mtupu, ni maneno ya plastic.Mkataba wa kundi ndio uliisha ila bado Supreme na Matalanta niwashikaji kwa sana ,alisema Planet kenya.Nukta Saba haitachoka kuwakumbusha wasanii watu kuwa mcheza kwao hutuzwa!

1 comment:

  1. Enter your comment...kabisaa wasanii wa malindi hawa supportiani kabisaa na bifu ndogo ndogo planet endelea kutupa mziki mzuri na milango mingi itazidi funguka

    ReplyDelete