Sunday, 31 March 2019

TETEMA MWANZELE LAUNCHING KULIENDAJE !


Nuktasaba wamepata nafasi kuhudhuria TETEMA MWANZELE LAUNCHING ya MR BAD0 hapo jana kule RADIO MARIA BAR-DONGOKUNDU.Kwa kweli show imebamba sana.Kumefika watu wengi ambao wametetema mwanzele style hadi chee.

Tumeweza kukuandalia baadhi ya photoz zinaonyesha vyenye show ilikuwa imebamba hadi watu wanaTETEMA mwanzele style.

Pia kulikuwa na video shooting ya hii nyimbo ambayo huenda ikaachilia hivi karibu maybe mwisho wa hii wiki tuliyoianza leo lakini tunafatilia tukijua ni lini tukupasha.

TIMATSI KUACHILIA NGOMA MPYA.




Taarifa tuzipatazo toka kitengo chetu ni kwamba ifikapo kesho tarehe 1/4/2019 msanii mkali wa MOZTACH REKORDZ ataachilia mpini mpya kwa jina WATAKUGANDAMA.Ngoma hii yenye mdundo mkali huenda ikafanya vizuri sana sababu itaachiliwa na rasmi na RADIO JAHAZI chini ya kipindi kitakachosimamiwa na CAPTAIN DAVID MAFISH.Kwa kweli hii ni zaidi ya redio kwenye masafa ya 87.7 Fm jinsi vyenye hudondosha mziki wa wasanii waliobobea kizazi yaani wenye majina na pia vyenye inapromote muziki wa nyumbani.Kaa mkao wa kula usubiri kazi ikidondoka tu uipate hapa.

DJ MWAS 254 ADOKEZEA NUKTASABA "BANGO LIVE@ RED LION CLUB"



Dj MWAS amekutana na Nuktasaba katika show flani inayoendelea saa hii katika eneo la burudani mjini ( jina limebanwa)na kuiarifu kwamba tarehe 6/4/2019 kutakuwa na BANGO LIVE likiwakilishwa na HOSINI  BAND na BRASSO.Sheshe hii itakuwa ni Wedding Extension .Halafu pia DJ MWAS ameiambia Nuktasaba kwamba hiyo siku ataachilia mixx kali za kufa mtu .Amedai mix hizo zitabamba crowd vinoma na pia itakuwa ni SCHOOL's OUT BASH .Kiingilio itakuwa ni mia mbili tu.200/=.

Usikose kufika..!!#KARIBU

Saturday, 30 March 2019

TUKUTANE BUDHAAZ LOUNGE AFTER ALASKAN GROUND#CHURCHILL SHOW


Watu wa Malindi City Leo Tukutane Apa BUDHAAZ  LOUNGE  baada ya show ya CHURCHILL kuisha after 11pm.KARIBUNI

FASH P KUKINUKISHA HIVI KARIBUNI!

Ni dhahiri kwamba Msanii mkali kutoka Pwani ya Kenya Fash P anapanga kuachia kazi mpya.Kutokana na post zake za hivi karibuni katika mitandao ya kijamii,msanii huyo ameonyesha kuwepo kwa kibao kipya.Bado haijabainika kama Rapa huyo anapanga kumshirikisha msanii yupi na anafanya kazi hiyo mpya studio gani ila tunavyojua kama NUKTA SABA nikwamba msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wengine wanaofanya kazi zao Crack Sound Records mjini Kilifi.


Hatutashangaa sana pini hilo likitoka Crack Sound na likiwa limefanyiwa kazi na wakali kama Jay Crack , Dhilly Dhilly ama CRASH V ambaye pia alimshirikisha kwenye ngoma yake inayoendelea kufanya vizuri kwenye anga za +254.Gonga Pia ndiyo ngoma ambayo Fash P alimshirikisha CRASH V iliyotayarishwa na Dhilly Dhilly .Unaweza kutazama video HAPA ama pia upakue audio HAPA .NUKTA SABA itazidi kufuatilia na kukujuza kila linalojiri kuhusiana na kazi hii mpya.Tukae mkao wa kula kijanja kwa kuSUBSCRIBE kwa channel yake  HAPA

Friday, 29 March 2019

CONFUSER J NA KAZI MPYA


Msanii Confuser kaachilia mpini mkali jana .Ngoma hiyo kwa jina CHOZI LA KADZO inaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki mitandaoni.Nyimbo hii huenda ikasumbua anga za burudani sana hapa pwani na Kenya yote kwa jumla.Msanii huyo wa kike pia Leo usiku atawakilisha huko malindi kwenye CHURCHILL SHOW itakayofanyika hapo ALASKAN GROUNDS .Kwa kweli huyu msanii anaweza na tunaamini kwenye hiyo show ya baadaye jioni atafunika.Ukitaka kuipata audio mpya ya CHOZI LA KADZO ipate hapa https://youtu.be/ljIf3JFtYmo

Tukutane kwa CHURCHILL SHOW.!!

Thursday, 28 March 2019

LAUNCHING TETEMA MWANZELE


Nuktasaba inakuarifu kwamba tarehe thelathini huu mwezi 2019 yaani Jumamosi 30/03/2019 kutakuwa na Official Launching ya TETEMA MWANZELE SONG YAKE MR BADO apo ndani ya RADIO MARIA BAR iliyoko hapo DONGOKUNDU-WATAMU.Pia kutakuwa na VIDEO SHOOTING ya Nyimbo hiyo.Kutakuwa na RADIO KAYA ndani ya nyumba.Kutakuwa na uwepo special wa MZEE NYERERE KHONDE mwenyewe akiambatana na NYERERE JUNIOUR.NUKTASABA watakuwa ndani ya nyumba.Kiingilio ni bure.Usikose kufika kwenye sheshe hili #KUJA TETEMA na wenzako.Usisahau kusubscribe channel ya yutube ya MR BADO ili uwe unadondoa kazi zake mpya pindi aachiliapo.Nenda hapa https://youtu.be/b0b1sv8I598

Tuesday, 26 March 2019

SHEHEREKEA BIRTHDAY NA STAR


Mariah Carey ni mwanamuziki wa marekani .Alizaliwa siku kama ya leo.Alifanya muziki style ya pop.Alihit na vibao kama Vision of Love,Touch my body na zinginezo kibao.Aliolewa na Tommy mottola(1993-1998).Baadaye akaolewa na Nick Canon.Aliuza nakala mamilioni albamu ya We belong together.Amefikisha miaka aroibaini na nane.(48years).Alizaliwa Long island ,New York.
Tunawatakia wote wenye wamezaliwa siku kama ya Leo #HAPPY BIRTHDAY na MAISHA MAREFU.
@Nuktasaba

KILIFI GOT TALENT RELOADED

Kilifi Got Talent Reloaded Show imerudi tena.Itafanyika tarehe 29 mwezi wa machi 2019 huko DISTANT RELATIVES ,ECOLOGY  & BACKPACKERS .Kutakuwa na show ya kukata na shoka ikiwemo ya Staa PROFF,MEDALLION,LIL MIZEE,ZILLER BAS na wengine wengi.Kiingilio ni 200/=ama kundi la mtu 10 kwa 1000/=.Pia kutakuwa na show mbalimbali za kukuburudisha.
Usikose Kufika#Karibu

TETEMA MWANZELE STYLE


MR BADO ameachilia nyimbo mpya inayoitwa TETEMA .Inaendelea kushangaza mashabiki sababu nyimbo hii iko style ya mwanzele.Raundi hii ni watu wacheze TETEMA mwanzele style.Kwa kweli msanii huyu ni mbunifu sana sababu mashabiki wamezoea nyimbo ya TETEMA iliyofanywa na DIAMOND na VANNY BOY toka Tanzania sasa saa hii wanaTETEMA mwanzele style.Ukitaka kuiskia idondoe hapa https://youtu.be/b0b1sv8I598

Sunday, 24 March 2019

MIKE PLANET ASHAACHILIA TOTO BADI


Msanii MIKE PLANET ashatimiza ahadi yake kwa mashabiki wake ameachilia kichupa kipya moto sana kwa jina TOTO BADI.Ngoma hiyo inayozidi kuingia mitandaoni kwa sasa inazidi kupokelewa na kukubalika na mafans.Ukitaka kuiskia idondoe
https://mdundo.com/song/1302706

#BigUp@NuktaSaba.

TRILLIONAIRE KAENDA SOUTH AFRIKA#TETESI



Mkali wa Freestyle wa Pwani Kaskazini TRILLIONAIRE katimba South Africa kwa sasa kwenda fanya kazi na GODFATHER PRODUCTIONS kama tunavyozipata habari kutoka kwa kitengo chetu.Stori hii tunayoifatiliza kama ni ukweli basi TRILLY akifaulu kufanya kazi na vigogo hao atakuwa ametoboa kimuziki hapa Afrika na dunia nzima kwa jumla.Ripoti inayoendelea kutupa maswali ni je AUDIO anayotaka kuifanyia video aliifanya studio za KENYA ama ataifanya akiwa nchini SOUTH AFRICA ?Kusema kweli TRILLIONAIRE raundi hii amejituma sana hadi kuamua kufanya muziki wake kimataifa kwani ni wasanii wachache waliofanyiwa kazi na kampuni hii ya GODFATHER PRODUCTIONS
na zikafanya vyema akiwemo DIAMOND PLATINUMZ,MR FLAVOUR na wengineo.Kwa sasa tunamfatilia TRILLIONAIRE kama aliambatana na nani kwenye safari yake walioko kwenye Hotel moja ya kifahari mjini JOHANNESBURG wakijipanga kuanza kazi.Tunamuombea TRILLIONAIRE mafanikio huko SAUZI AFRIKA azidi kupeperusha jina la KENYA kote duniani.Kwa updates za muziki zipate hapa kwa blog yetu

Friday, 22 March 2019

MIKE PLANET KUACHILIA MPINI#

Msanii mkali anayefahamika kwa jina MIKE PLANET ameipa habari Nuktasaba kwamba ifikapo tarehe 25th March 2019 ataachilia ngoma rasmi.Nyimbo hiyo kwa jina TOTO BADI huenda ikafanya vizuri sana sababu produsa MASTER BRAM wa W.M.D RECORDS aliishuhulikia kwa ustadi.Isitoshe na MIKE PLANET ni msanii mwenye kujiamini .Tukae mkao wa kula sababu ikiachiliwa tu utaipata hapa Nuktasaba.

Thursday, 21 March 2019

DJ MWAS 254 AHOJIWA NA NUKTASABA



Nuktasaba imekutana na DJ mkali wa kazi DJ MWAS 254 leo .Hii imekuwa mwendo wa masaa ya mchana wakati ripota wetu alikuwa ameenda mtaa wa Watamu maeneo ya beach kikazi.Amebahatika kukaa na DJ MWAS 254 na wakalonga kwa muda.Mahojiano yamekuwa kama ifuatavyo...

Ripota: Vp mkali

Dj Mwas 254: Nko safy inakuaje ?

Ripota:Unapiga muziki club gani hapa Watamu ?

Dj Mwas 254:Club ninayowakilisha kwa sasa inaitwa RED LION iliyoko hapo Timboni opposite Total petrol station

Ripota:Ushawahi kuongoza show ya msanii yupi maarufu ?

Dj Mwas 254: Nishafanya kazi na wasanii wengi maarufu.Wa kwanza ni MR BADO ambaye nilimfanyia mara kadhaa show babu kubwa sana,wa pili ni KALICHA ambaye show yake ilikubalika sana na mashabiki na wengine wengi haki siezi maliza kutaja wote.

Ripota:Ok.Nakubali wewe unakaa unaweza kazi morale sana.Nkiulze sasa ,saa hii uko huku baharini (beach-jina limebanwa) umekam una.appointment na  mama mzungu nini ?

Dj Mwas:Mimi hujipenda sana mwanzo hujirusha kama mida inakubali.Ingekuwa ninadate na kinyanya cha kizungu ningekuwa saa niko ndani ya 5 star hotel nakula sheshe.

Ripota:Wazi.Hiyo ni sawa.Asante kwa muda wako na Nuktasaba.


Baada ya hapo ripota wetu amekatisha mahojiano.Wakaongea stori mob but kwa saa i wamezibana chini ya maji.Tutakupa stori uzidi kujua mengi kumhusu DJ MWAS 254 so zidi kufatilia Nuktasaba upate kujua usiyoyajua !  #Karibu


Wednesday, 20 March 2019

SAUTISOL NDANI YA MALINDI...


Ifikapo ijumaa tarehe 22 machi 2019 njia zote za MALINDI zitaelekea STARDUST DISCOTHEQUE kutakakokuwa na show ya kundi zima la wazee wa kazi SAUTISOL watakaowakilisha .Kundi hili maarufu sana KENYA nzima limefanya kazi na wasanii tofauti ulimwenguni ikiwemo PATORANKING,YEMI ALADE na wengineo kitu kilichoinua jina la KENYA mbali sana kimuziki.Pia kutakuwa na msanii KALICHA anayeendelea kufanya vizuri nchini .

Ukitaka kuona show ya kukata na shoka ya SAUTISOL na KALICHA fika STARDUST DISCOTHEQUE #NjooUjionee#

CHIKUZEE NA NGOMA MPYA.#

Msanii mkali wa pwani kwa jina " CHIKUZEE" ameachilia ngoma mpya leo inayofahamika kama "I LOVE YOU".Msanii huyu mzee wa mavuvuzela jina lake lingine la fani ametengeza kibao hiki studio ya MK 2 STUDIO .Mzuka huu huenda ukafanya vizuri sana sababu CHIKUZEE habahatishi kwenye kazi zake akiachilia bomba ni tindo.Kwa kweli hakuna asiyemjua kwani ametawala anga kenya mara nyingi kwa ngoma kama vile NGOMA ITAMBAE aliyomshirikisha SUSUMILA,HIDAYA,KICHUNGU zikiwemo nyinginezo.Ngoma hii tunamuombea CHIKUZEE izidi kupokelewa vizuri na mashabiki wote.Ukitaka kupata ngoma hiyo idondoe hapa https://mdundo.com/song/1290943?fbclid=IwAR1xAz7dqnZYHSFM1F3JrBhwI2NyhzZAkOpC4krusrTwKBVFYJ5XdjrSu1Y

Tuesday, 19 March 2019

FASH P, MEDALLION ,TRILLIONAIRE NA NUKTASABA

Wasanii hawa vigogo wa sanaa KILIFI COUNTY wamekutana na kitengo chetu na kuongea kwa marefu kuhusu kazi zao mpya na baada ya mkao kuipa NUKTASABA  links washare kwa mafans ili wadondoe kazi zao mpya kwa urahisi.Hii itakuwa nafasi mzuri kwa mafans kupata kazi zao mpya zinazogonga mitandao kwas sasa.

Kazi za FASH P zipate kwa links hizi....


 GONGA PIA _-FASH P FT CRASH V OFFICIAL VIDEO 👉🏼 https://youtu.be/pBN-UUdN3Co
#GongaPia SUBSCRIBE 👉 https://www.youtube.com/channel/UCL-Gnq96Y0CoyQCpYIVuTjQ

GONGA PIA _-FASH P FT CRASH V OFFICIAL AUDIO 👉 https://mdundo.com/dl/1285134/low

ViuSasa 👉 Gonga pia https://viusasa.com/music/play/viausrx

Kazi za MEDALLION  zipate kwa links hizi....


New hit song  *titled *Karakara*🔥🔥🔥
https://youtu.be/KlLkXjCA05I

Kwa kazi mpya ya TRILLIONAIRE na C.B.K

idondoe hapa
https://youtu.be/VZ5SNoq7pDw
Motooo 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

Monday, 18 March 2019

TIMATSI APUUZA TETESI.


Leo ,Nuktasaba tumepambana na msanii wa MOZTACH TIMATSI na tulipomhoji kuhusu tetesi zilizopo juu yake amepuuza umbea wa kwenye mtandao ati anasakwa na polisi kisa ni kufanya video ya ANANESA na mtoto wa  kike wa miaka 16.Amedai hizo ni tetesi tu za vibaka wake wasiopenda ang'are na azidi kufanya vizuri kimuziki.Tulipomuuliza alikuwa wapi mbona kajichikia chini ya maji kwa muda sasa amedai alikuwa  amesafiri kiasi kwenda tayari kazi mpya atakayoiachilia hivi karibuni.Ameisifu itagonga vichwa zaidi ya ANANESA.So tusubiri kazi hiyo ikidondoshwa tu utaipata hapa.

Sunday, 17 March 2019

MEDALLION ALIONGOZA NAMBA 1.

Habari tuzipatazo kwa saa hii ni kwamba SHOW YA KILIFI GOT TALENT ilifanyika vyema jana na   MEDALLION ndio alikuwa wa kwanza yaani namba moja   nakuondoka kitita cha 50k.
Akafatiliwa na msanii,namba mbili ZILLER BUS aliyeondoka na 30k(elfu thelathini).Namba 3 akachukua LIL MIZZE aliyetoka na 20k.

Show hii ya jana ilidhihirisha KILIFI COUNTY kuna vipaji na wasanii wanaweza.#TUNAKUZAVIPAJI#

WATU ZAIDI YA MILIONI MOJA WAMESHACHUKUA SELFIE!

Campaign iliyohusisha washikadau mbali mbali wa mziki nchini Kenya iliyojulikana kama #Playkenyanmusic ama #Playke ( Play Kenyan Music ) imedhihirisha kuwa na msukumo wa aina yake.Ilileta gumzo nchini na hata mataifa jirani ikiwemo Tanzania issue ikihitajika media zote nchini Kenya kucheza asilimia kubwa ya kazi za nyumbani.Campaign hii pia imepelekea kuona wasanii tajika kuja pamoja na kufanya kazi bab kubwa ili kuonyesha uwezo wa vipaji vya humu nchini.


Project iliyowaleta wasanii Khaligraph Jones,Fena, Jua Cali,Nyashinski na Naiboi inayojulikana kama CHUKUA SELFIE imegonga views zaidi ya 1.5 Million ndani ya wiki moja! I say KENYA uwezo upo asikwambie mtu.Chukua SELFIE pia wewe https://youtu.be/vDih4Rq_Fto

Saturday, 16 March 2019

BURUDANI WATAMU



Wasanii wakongwe kwa hii tasnia ya kizazi kipya, LONGOMBAS wameonyesha dalili za kurudi tena kwa game.Hii ni baada ya kusambaa kwa mabango ya kuwa watakuwa wanakinukisha ndani ya mji wa kitalii wa Watamu. Longombas wanakumbukwa kwa vibao kama vile Dondosa,Piga Makofi ,Vuta Pumz na Shika more.Watu wa Kilifi Kaskazini wanayo nafasi ya kuVuta Pumzi na wasanii hao usiku wa tarehe 30 mwezi wa 3 mwaka huu! Itakuwa shangwe ndani ya Coconut Beach Watamu.Tukutane basi tupige maselfie wa wakali wa kanda hiyo wakiwemo Kina Fash P,Trillionaire,Lil Mizze,S.D.I,Tmatsi,N.Ricky,Klean Heart,Ak Genious na wengine kibao watakao pagawisha kwa freestyle za nguvu kuwaribisha nyumbani ndugu hao Lovi na Christian Longomba.Bila kusahau NUKTA SABA pia tutakuwa ndaaaani! Ndio hivyo basi..

TRILLIONAIRE AMEKANUSHA TETESI


Nuktasaba imekutana na TRILLIONAIRE leo  kwenye maktaba moja mjini na alipoulzwa kuhusu tetesi iliyopo mitandao,akajibu hivi " Mimi ni msanii mkongwe ninayejiheshimu na huwa naheshimu vitu vya watu so mimi siwezi kuwa uhusiano na bibi ya mwenzangu kisa ni pombe".akaongeza " Hiyo labda ni mahasidi wangu wanaotaka kunichafulia jina kwa mtandao lakini hawataniweza ".Ameahidi anaendelea kusukuma ngoma zake ikiwemo ENERGY inayomuongezea umaarufu na inazidi kukubalika na mafans wengi.Kwa habari  latest za muziki tembelea blog yetu.

Friday, 15 March 2019

ARROW BWOY NA DEMARCO TENA.


Msanii wa Nairobi ameachilia ngoma na mkongwe wa Jamaica mkali wa kazi DEMARCO.Track hiyo inapokelewa vizuri kwenye mitandao.Mpini huo unaitwa LOVE DOCTOR unagonga anga tangu uachiliwe mapema leo.Hii ni ishara ya ukali wa kuonyesha ARROW BWOY ni INTERNATIONAL ARTIST kwa sasa.Mwezi uliopata alifanya kazi na CECILE .Saa hii DEMARCO,si uongo ARROW BWOY ni MOTO wa kuotea mbali.

Thursday, 14 March 2019

MEDALLION AMERUDI TENA !


Mkali wa kazi yaani dingi wa masauti toka kilifornia city kwa jina MEDALLION amerudi tena.Msanii huyu alietingisha anga na track ya IVO IVO ametangaza ujio wake tena bamba mpya tena kwa jina KARAKARA ambayo ataichia tarehe kumi na sita mwezi wa tatu 2019.Amedai nyimbo hii itawaacha hoi mashabiki akiiachilia hapo siku ya jumamosi.Tulipomuuliza kuhusu zile picha alizopost kwa mitandao wiki iliyopita zilizoleta tetesi kuwa huenda akawa amejiunga na chama cha ILLUMINATI alidai ni mbwembwe tu za watu ,yeye ni mtu wa bidii zake hategemei  nguvu za giza.Track hiyo iliyoundwa na produsa DHILY DHILY huenda ikafanya vizuri sana sababu imekaliwa na mkali wa kazi.Ikidondoshwa tu utaipata hiyo nyimbo hapa kwa blog yetu.#Usikae mbali

Wednesday, 13 March 2019

TRILLIONAIRE KAFUMANIWA ! JE NI KWELI ?#TETESI


Mkongwe wa freestyles na punchlines kafumaniwa na kidosho.Tukio hilo tunalolifatilia imedaiwa TRILLIONAIRE amenaswa na kidosho huyo anayemilikiwa na mzungu mmoja tajiri mwenye BAR fulani maarufu sana MALINDI(jina limebanwa) leo asubuhi.Ripota wetu ametuarifu gwiji huyu ameponea mauti sababu mzungu ametaka kumpiga risasi lakini akaogopa kadamnasi ya watu walioshutushwa na kelele mwendo wa asubuhi.Inasemekana TRILLY alikuwa yuko kwenye chumba cha Guest ya Bar akila uroda ndipo mzungu akashtuka kipenzi wa amepotea.Akajaribu kumtafuta eneo lote la burudani akamkosa.Ndipo mlinda geti mmoja akamwaga mchele kusema mrembo huyo ameonekana mwisho akinywa mvinyo na staa huyo ambao walikuwa karibu sana kwenye meza moja wakilana denda na kutokomea nyuma ya bar kwenye Guest rooms.Ikabidi mzungu kuanza kumtafuta chumba baada ya chumba.Ndipo hapo TRILLIONAIRE kashikwa akila asali ya wenyewe.Baada ya kisanga hicho mpambe ameingia mitini kwani wanahabari wa magazeti na maredio walikuwa wamewahi hapo kumhoji kunaendaje ?Kwa sasa tunatafuta ukweli wa stori hii so tunaomba alipo TRILLIONAIRE ajitokeze afunguke aanike ukweli. @~kiki~

VIDEO YA NAJIDAI IMETOKA RASMI LEO


Msanii SEE FAR ameachilia video ya nyimbo kwa jina NAJIDAI  rasmi leo.Video hiyo imeundwa na MOZVIDEOZ imeundwa kwa ustadi sana na huenda ikafanya vizuri sana .Video hiyo iliyongojewa na mashabiki sasa iko kwa mtandao live.Ukitaka kuidondoa ipate hapa https://youtu.be/DC1C_6_hgfk .Tunamuombea SEE FAR mafanikio.

Tuesday, 12 March 2019

SEE FAR KUACHILIA VIDEO MPYA..


Msanii mkali wa MOZTACH RECORDS kwa jina SEE FAR ataachilia video mpya kwa jina NAJIDAI ifikapo kesho tarehe 13/03/2019.Video ya nyimbo hiyo kali itaachilia pamoja na track NAJIDAI so usiwe mbali kuipata na kuiona hapo kesho.Video hiyo iliyosubiriwa na mafans kwa muda mrefu huenda ikafanya vizuri sana.Tutakuekea link ili uweze kuidondoa hapa kwa blog yetu.Ukitaka kupata habari latest za sanaa tembelea blog yetu#Nuktasaba

Monday, 11 March 2019

VIDEO YA AUDITIONS ZA JANA NJE..


Nuktasaba iliwahi kuwepo kwa auditions za talent search hapo jana ukumbi wa DE COFFEE PUB -TITANIC KILIFI na tuliweza kupata video ya chipukizi jinsi walivyohemeshana kwenye MIC kila mmoja kuwa mkali za yao.Kwa kweli show ya jana ilibamba sana sababu kila mtu anataka ustaa.Show hiyo ilikuwa ni Auditions tu but ifikapo 16th huu mwezi huko Bofa beach vidazini -Kilifi tutawajua wakali .Ukitaka kuona video jinsi auditions ilivyokuwa ipate https://m.youtube.com/watch?v=uX3Vg8Q4_1A&feature=youtu.be.Ukitaka kupata updates za sanaa tembelea blog yetu

Sunday, 10 March 2019

TIMATSI ANASAKWA NA POLISI..#TETESI


HABARI TUNAZOPATA TOKA KWA KITENGO HICHO NI KWAMBA TIMATSI ANASAKWA  NA POLISI .STORI HIYO TUNAYOFATILIA KOSA LA MSANII HUYO NI KUWA NA MTOTO WA KIKE WA MIAKA 16 KWENYE VIDEO YA ANANESA.HILO LILIDHIHIRISHWA NA KUSAMBAA KWA VIDEO HIYO KWENYE MTANDAO AMBAPO UKANDA HUO ULIONEKANA NA WAZAZI WA MSICHANA HUYO. ILIBIDI WAZAZI WA MWANAFUNZI HUYO KUFIKA SHULE NA KUJA KUFATILIA STORI HIO.ILIWABIDI WAMPELEKE POLISI MSICHANA HUYO NDO AKATOA UKWELI  .ILIBIDI MWALIMU MKUU WA SHULE HIYO(JINA LIMEBANWA) KUMCHUKULIA HATUA  YA KISHERIA MLINZI WAKE SABABU ALIMRUHUSU MWANADADA HUYO KUTOKA USIKU WAKATI AMBAO VIDEO HIYO ILICHUKULIWA.KWA SASA TIMATSI YUKO MAFICHONI SABABU ALIHARIBU MTOTO WA SHULE.MLINZI PIA AKO KOROKORONI.MSICHANA ALIACHILIWA AKARUDI SHULENI LAKINI INASEMEKANA AMEKOSA KUINGIA DARASANI KWA WIKI YOTE ILIYOPITA.INASHUKIWA HUENDA TIMATSI ALIMPACHIKA MIMBA !JE NI KWELI ? HILI NI BAADHI YA MASWALI ENDAPO TUTAMKUTA TIMATSI ATATUPA JIBU LAKE ! ENDELEA KUFATILIA STORI HII HAPA NUKTASABA TIMATSI TUKIMPATA ITAENDELEA...

Saturday, 9 March 2019

FASH P APATANA NA NUKTASABA



FASH P amepatana na Nuktasaba na kuwapa updates zifuatazo.
🚨Wiki ya kuanzia 25th this month video ya GONGA PIA _-FASH P FT CRASH V  itakuwa inaonyeshwa Mseto East Africa @Citizen TV the whole week.Pia ukitaka kupata videos zengine za FASH P unaweza kuzipata hapa https://www.youtube.com/channel/UCL-Gnq96Y0CoyQCpYIVuTjQ
Chakufanya mwanzo TAZAMA ,LIKE ,SHARE & SUBSCRIBE.Enjoy.!!!

Friday, 8 March 2019

MWANZELE NIGHT


Nuktasaba inakualika kesho kwa bonge la party ndani  ya WHITE ROCK  iliyoko hapo JIWE LEUPE-WATAMU.Kutakuwa na mkongwe wa kazi MR BADO atakayetumbuiza na midundo ya MWANZELE hadi chee.Pia kutakuwa na CHAMA NYOMA free kwa MWANZELE FANS wote.Hii si ya kukosa.Njooni nyote tujivunie utamaduni wetu.
KARIBUNI !!

Thursday, 7 March 2019

LANGE MWEPESI AKUTANA NA NUKTASABA



Msanii wa Kilifornia yaani mkongwe wa kazi anayejulikana kwa STAGE NAME ya LANGE MWEPESI amekutana ripota wetu na kumpa habari njema kwamba ifikapo next week anaenda shoot video kwa sango under Marvin brudhas na kuna kitu moto ameiandaa inaenda kwa jina la "USHANITEKA".  Audio iko tayari Ila mwaka huu anataka kuenda tofauti kiasi yaani mwendo wakuachia singo na video itakua hatua nzuri pia katika soko la muziki. , Bamba zuri lishapikwa chini ya uangalizi wa AYK records under SANGO producer...Alipoulizwa ana ujumbe gani wa mashabiki amedai hivi "Nawambia mashabiki wangu na wa Gallant Pasasha kwa ujumla wakae mkao wakisubiria kazi nzuri na yenye ujumbe bora So hapa kwenye anga za NuktaSaba ndio mtapata habari zote,kuna kazi nyingi nzuri na zaidi ya moja ziko njiani zinakuja so.asanteni kwa upendo " #Ovaaaa✊

NANI MKALI KILIFI"TUNAKUZA VIPAJI "



KILIFI GOT TALENT 2019

A SEARCH FOR THE BEST SINGER

1st  prize Ksh. 50,000/=
2nd prize Ksh. 30,000/=
3rd  prize Ksh. 20,000/=
Plus
• Record deal
• Video clip
• Promotion
• Tour

AUDITION ON 10TH MARCH AT DE COFFEE PUB KILIFI. (TITANIC HOTEL)
TIME: 10:00AM TO 2:00PM

COMPETITION ON 16TH MARCH AT VIDAZINI BEACH (BOFA) KILIFI.
TIME: 10:00AM TO 4:00PM

Get Discovered and be Nurtured to Stardom.

MEDALLION ANATAFUTA KIKI AMA...# ??

Msanii mkali wa CRACK SOUND RECORDS kwa jina MEDALLION ametafutwa na ripota wetu ahojiwe kuhusu tetesi zinazoenea kwa mtandao kumhusu.MEDALLION amefanya vizuri sana kwenye vyombo vya habari .Ikizingatiwa nyimbo zake kama vile IVO IVO ,KITETE na zingine mingi zimetawala anga za burudani kama vile  Kaya Fm,Jahazi Fm,Pwani Fm,Bahari Fm na zinginezo.Cha ajabu kinachogonga mitandao ni posts za MEDALLION mitandaoni.Siku hizi anaeka picha za kiajabu sana.Si makosa msanii kuwa mtanashati,inaruhusiwa awe smart,aende na fashion,avae pete mob za silver ama magoro kifuani.Cha ajabu msanii huyu amezidi kwa hili sababu posts zake siku hizi zinawapa mafans maswali.Kwa ukweli siku hizi kuna alama zingine ukizionyesha kwenye posts mashabiki unawapa maswali magumu kukuelewa.Kuna mashabiki wengi huleta tetesi kwenye mtandao kuwa msanii huyu huenda anafanya harakati zengine ambazo si za maadili ama yuko mbioni kutafuta ufanisi kwa mkato.Hii ndo sababu MEDALLION anatafutwa na ripota wetu aeleze kuhusu hili.Kwa ufupi MEDALLION jitokeze ufunguke kwa mafans wako hata kama pia ni kutafuta kiki pia itaeleweka tu.
Kwa habari latest za muziki zipate hapa.

Wednesday, 6 March 2019

TRILLIONAIRE AFUNGUKA " ALIKOTOKA NI MBALI"




Rapper  mkali wa michano amepatana na ripota wa Nuktasaba na akafunguka kuhusu safari yake kimuziki.
Alianza muziki mwaka 2011 studio ya BIANCA NERO iliyoko TIMBONI ~WATAMU.Alifanya nyimbo kwa jina "RESPECT ME".Track hiyo aliifanyia video .Nyimbo hii ilipenya hewani kwa muda lakini haikuweza sana .Hii ilimfaɲya Rapper huyo kukaa chini kuandika mkoko mwingine kwa jina DIGITAL.Mpini huu aliufanyia video na kuupa kiki iliyofanya ufanye vizuri kwenye Radio Kaya,Pwani Fm na Bahari Fm.Video pia ilipenya kwenye stesheni za televisheni ikiwemo Pwani Tv.Mnamo 2014 TRILLIONAIRE alihamia MOZTACH RECORDS chini ya produsa MOZ.Tulipomuuliza Rapper chanzo cha kuhamia akadai alikubali sana kazi za MOZ na akajua Produsa huyo angemfaa sana sababu ngoma zake zina hisia kama za Rapper huyo so akaamini kwake amefika.Hapo alifanya nyimbo kwa jina "TAKE IT EASY".Nyimbo hii haikufanya vizuri sababu ilikosa hata video.Hii ikambidi arudi tena studio na kutoa kibao kipya kwa jina LOOSE CONTROL.Mpini huu alimshirikisha msanii wa kike kwa jina BEAUTIFUL SOPHY.Nyimbo hii ilikubalika mitandaoni na kwa maredio sababu ilikuwa na video iliyoweza.Hapo Rapper huyo alijulikana sana na akaanza kupata shows kwenye kumbi za burudani ndani ya Watamu na Malindi.Trillionaire akatoa kibao chengine na PC LEE kwa jina MUWEZA NI MAANANI.Kibao hiki kilimfanya akatamba sana sababu alikifanyia Video iliyogonga vichwa vya burudani kwa ukali wake.Ilipofika 2018 akaachilia mpini kwa jina NIKUITE NANI.Bomba hili alifanya video iliyozidi kumpa jina kubwa pwani na Kenya yote .Ngoma hii ilitamba Radio Kaya,Pwani Fm,Baraka Fm na Bahari.Ngoma hii iliongeza umaarufu wake Rapper huyu Mkali.Ilipofika 2019 aliachilia kichupa kwa jina "ENERGY".Ngoma hii aliiachilia na video yake kali sana.Video hiyo iling'ara sana na tulipomhoji TRILLIONAIRE alidai alitumia nusu millioni(Kshs) kuitayarisha.Tulikubali sababu iliundwa kwa umakini na ina scenes nyingi bab kubwa zilizohitaji garama ya juu.Rapper huyo alidai huu ni mwaka mpya na ni mwanzo mpya so inabidi afanye mambo makubwa ili jina lake lisishuke.Alidokezea ripota wetu kuwa ameandikisha mkataba na MOZTACH RECORDS ili asibatishe afanye kazi kiukweli.Tarehe Moja machi 2019, aliachilia mpini mwengine mpya kwa jina " BAD GAL".Mpini huo unafanya vyema sana yaani mashabiki wanaupokea sawa haswa video yake inavyoshika uionapo.Ukitaka kuiona idondoe hapa   https://youtu.be/UV9bUVEwlcA.TRILLIONAIRE ameahidi mashabiki wake huu mwaka anapanga kazi zitakazoteka soko la East Africa na kuitawala.Amedai sa hii anaachilia HIT baada ya HIT kwa wakae mkao wa kula wakisubiri HITS.Tunamuombea TRILLIONAIRE mafanikio.

Tuesday, 5 March 2019

FASH P NA CRASH V WANATAMBA NA GONGA PIA.


Rapa mkali wa HIPHOP kutoka NORTH COAST anatamba na video ya nyimbo kwa jina "GONGA PIA" aliyomshirikisha mkali wa kazi CRASH V.Video inaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki.FASH P alizidi kupandisha mzuka kwenye track jinsi mistari ilivyonata na beat na wingi wa punchlines .Kwa kweli nyimbo hii inavuma mitandaoni na maredio za pwani zikiwemo JAHAZI FM ,KAYA FM,BAHARI FM NA PWANI FM.Ukitaka kutazama video hiyo idondoe hapa https://youtu.be/pBN-UUdN3Co

TRILLIONAIRE AKUTANA NA NUKTASABA


Msanii mkali wa styles kutoka MOZTACH RECORDS amekutana na  Ripota wetu wa Nuktasaba na amehojiwa akaongea na Ripota wetu akajieleza stori mob kumhusu so usiwe mbali utazipata hapa kwa  blog yetu.

TIMATSI AACHILIA VIDEO MPYA



Msanii mkali kutoka MOZTACH RECORDS studio ndani ya G TOWN CITY  kwa jina TIMATSI ameachilia video ya ngoma ANANESA.Ngoma hiyo inayoendelea kufanya vizuri kwenye Radio za pwani zikiwemo Kaya Fm ,Jahazi Fm,Pwani Fm na Baraka Fm.Msanii huyu aliyeanza muziki 2010 kwenye studio ya TEE HITS na nyimbo iliyoitwa TIMATSI .Nyimbo ilivuma 2011 kwenye Redio Kaya,Pwani Fm na Baraka Fm lakini haikufanya vizuri kwa sababu ilikosa kufanyiwa video. 2011 alienda GREEN HOUSE RECORDS akafanya kibao kiitwacho WOYOWIYE alichomshirikisha SHABIG na DOGO RICHIE ambacho pia hakikufanya vizuri.TIMATSI alijaribu kusukuma kazi hiyo lakini haikukubalika sana na mafans.Baada ya hapo ikabidi TIMATSI aende chini ya maji.Tulipomuulza kwa nini TIMATSI alikuwa amepotea akadai alikuwa amerudi shule ya upili sababu aliona kabla kutoboa ni muhimu mwanzo apate kisomo.Alipomalza kusoma alirudi tena studio mwaka wa 2018.Studio aliyojiunga nayo ni MOZTACH RECORDS ilimtoa na kibao kinachowika ANANESA.Mpini huu ameachilia na video yake iliyoundwa na  MOZTACH VIDEOz iko kali.Video hiyo imetawala sana mitandaoni na hii ni ishara ya TIMATSI kuliteka soko la muziki la EAST AFRICA.Ukitaka kupata video hiyo idondoe hapa https://youtu.be/KTCYgNKhwkU.Ukitaka habari latest za muziki tembelea blog yetu.