Msanii mkali kutoka
MOZTACH RECORDS studio ndani ya G TOWN CITY kwa jina
TIMATSI ameachilia video ya ngoma
ANANESA.Ngoma hiyo inayoendelea kufanya vizuri kwenye Radio za pwani zikiwemo Kaya Fm ,Jahazi Fm,Pwani Fm na Baraka Fm.Msanii huyu aliyeanza muziki 2010 kwenye studio ya TEE HITS na nyimbo iliyoitwa
TIMATSI .Nyimbo ilivuma 2011 kwenye Redio Kaya,Pwani Fm na Baraka Fm lakini haikufanya vizuri kwa sababu ilikosa kufanyiwa video. 2011 alienda GREEN HOUSE RECORDS akafanya kibao kiitwacho WOYOWIYE alichomshirikisha SHABIG na DOGO RICHIE ambacho pia hakikufanya vizuri.
TIMATSI alijaribu kusukuma kazi hiyo lakini haikukubalika sana na mafans.Baada ya hapo ikabidi TIMATSI aende chini ya maji.Tulipomuulza kwa nini
TIMATSI alikuwa amepotea akadai alikuwa amerudi shule ya upili sababu aliona kabla kutoboa ni muhimu mwanzo apate kisomo.Alipomalza kusoma alirudi tena studio mwaka wa 2018.Studio aliyojiunga nayo ni MOZTACH RECORDS ilimtoa na kibao kinachowika
ANANESA.Mpini huu ameachilia na video yake iliyoundwa na MOZTACH VIDEOz iko kali.Video hiyo imetawala sana mitandaoni na hii ni ishara ya TIMATSI kuliteka soko la muziki la EAST AFRICA.Ukitaka kupata video hiyo idondoe hapa
https://youtu.be/KTCYgNKhwkU.Ukitaka habari latest za muziki tembelea blog yetu.
No comments:
Post a Comment