Friday, 19 July 2019
'BADO RECORDS HAIWEZI MZIKI WANGU'
Msanii kutoka pwani ya Kenya,kaunti ya Kilifi anayekwenda kwa jina Timatsi ameiponda studio ya msanii mwenza Mr Bado iliyoko Watamu.Haya yametokea kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji Pascal Shanga na Mtu Bei kwenye kipindi cha Chachawiza ndani ya Bahari FM leo ijumaa tarehe 19.Timatsi amekiri kuwa studio ya msanii Mr Bado haina hadhi ya kumfanyia kazi zake kwa kuwa producer wa studio hiyo hajamakinika.
Ameongezea kwamba wakati alipokuwa chini ya himaya ya Bado Records, alikuwa akifanya tu mazoezi ya sauti yake ila hakuwa chini ya studio hiyo kikazi.Ikikumbukwa kwamba Timatsi ni msanii aliyekuwa miongoni mwa watu wa karibu wa Mr Bado na hata kuwa mwanachama wa KICOTA,kikundi kilichoanzishwa na Mr Bado.Kupitia mahojiano hayo,imebainika kuwa Mr Bado hakuwahi kufanya kazi zake kwenye studio yake ila kwenye studio za Crack Sound chini ya producer Jay Crack.Labda haya ndiyo yaliyopelekea kusambaratika kwa studio hiyo kwa kuwa kufikia sasa hakuna wasanii wanaofanya vizuri kutoka studio hiyo .Je ,studio hii imebaki kama mahali kwa kufanyia mazoezi kama alivyofunguka Timatsi ama alikuwa anaponda tu? Meza yetu ya habari inafuatilia habari hizi ili kubaini kama maneno ya Timatsi yana ukweli ama kuna mambo ya kibanafsi baina ya wawili hao.
CREW NDANI YA BAHARI FM
Wasanii wakali kutoka county 003 leo wako ndani ya BAHARI FM kuanzia 1PM hadi 4PM wakiwa na MTU MZIMA a.k.a MTU BEI a.k.a PASCAL SHANGA.
Show hii naaminia wakali hawa akiwemo SEEFAR,TIMATSI,TRILLIONAIRE,DOUBLE MIND na MOZTACH watafunguka live kuhusu safari yao kimziki.
Thursday, 18 July 2019
MOZTACH CREW WAKO JIJI KUANZA TOUR
Asubuhi ya leo tumefuatilia Team Moztach walioingia jiji usiku na wamedai tayari wameingia jiji kuanza media tour..Wapambe hao tuliweza kupata baadhi ikiwemo TRILLY,SEE FAR na TMATSI tukalonga nao wamedai tusiwe mbali na vyombo vya habari tuwategee leo.
Wednesday, 17 July 2019
MOZTACH CREW KWENDA NAIROBI..
Moztach crew tayari wameanza safari kwenda MEDIA TOUR NAIROBI.Crew hiyo akiwemo TMATSI,SEE FAR,TRILLY,DOUBLE MIND ,MOZTACH NA RED EYE wamepambana na ripota wetu wakiwa MOI INTERNATIONAL AIRPORT -Mombasa .Wamedai walikuwa wataondoka na ndege ya tatu usiku na kwa sasa nawawe washaanza safari.Tunawaombea mafanikio .!
Tuesday, 16 July 2019
Monday, 15 July 2019
MOZTACH CREW KUENDA MEDIA TOUR#
Wasanii wa kutoka jumba la muziki yaani TEAM MOZTACH kwenda MEDIA TOUR.Wakali hao akiwemo SEE FAR,TMATSI,DOUBLE MIND ,TRILLY na MOZTACH watakuwa NAIROBI CITY hii wiki kama ilivyoratibiwa wakifanya MEDIA TOUR ya kazi zao ambapo watatembelea BAHARI FM tarehe 19/07/2019 na tarehe 20/07/2019 watakuwa KBC RADIO TAIFA
na zinginezo.Usikose kusikia LIVE INTERVIEWS zao.Pia wataandamana na ACTOR RED EYES ambaye atakuwa ameenda kufanya Launching ya movie aliyoifanya kwa jina NGAO NA NGUMBAO.Launching hii atatembelea Tv stesheni kadhaa .Hii Media tour itasaidia kusukuma kazi za wasanii hawa mbele.#Goodluck
SWAHIB ANANICHELEWESHA ! N.RICKY ALAUMU .
Msanii wa himaya ya GLM anayejulikana kama N.RICKY ana lawama alizoelezea meza yetu leo.N.RICKY amefunguka akadai Produsa SWAHIB anayemiliki MASELLE RECORDS iliyoko RUIRU jijini NAIROBI amechelewesha kuachilia kazi yake kwa jina NILEWE aliyoifatilia kwa muda sasa.Kazi hiyo ambayo aliifanya mnamo february mwaka huu baada ya kuachia track NAJIUGUZA aliyofanya na FASH P, N.RICKY amefunguka kama ifuatavyo "SWAHIB amekuwa akinizungusha mara nyingi ,kila nkimpitia studio anadai bado hajamaliza,sasa ananichanganya .Sijamuelewa kuna nini ama shida iko wapi.Ama labda ni vyenye nimemshirikisha kwenye nyimbo hii ? Nyimbo hiyo ambayo nilikuwa nani.irelease tarehe 26/6/2019 lakini ikabidi niitulize kidogo sababu kuna FASH P C.E.O wa GLM ambaye alikuwa anaachilia track inayoitwa OK aliyomshirikisha CRASH V .Baadaye nkapanga tarehe 16/07/2019 yaani hapo kesho niachilie lakini sina hopes sababu SWAHIB simuelewi.Siku hii pia ningeadhimisha BIRTHDAY ya mtoto wangu.Afadhali angesema ningemuulewa " hivyo ndivyo N.RICKY alivyofunguka .Kusema ukweli SWAHIB sio poa kutoachilia kazi ya msanii wako sababu wasanii ndo wanaoinua jina la studio.Pia tumemushauri N.RICKY afatilize hii stori polepole. Tunamtafuta Produsa SWAHIB atueleze ukweli kuhusu swala hili.SWAHIB popote ulipo jua unatafutwa na NUKTASABA ufunguke pia bro.
Subscribe to:
Posts (Atom)