Ifikapo kesho tarehe 5/5/2019,DHILLY DHILLY na ZERE LA MAPOZI a.k.a MCHAFUZY watakuwa ndani ya Radio Kaya wakihojiwa live .Kupitia mahojiano hayo utaweza kujua mengi kuwahusu vichwa hawa wawili wa KILIFONIA CITY.Usikose kutegea hapo kesho.!
Saturday, 4 May 2019
WALK AWAY TOUR KUFIKA RADIO KAYA
Ifikapo kesho tarehe 5/5/2019,DHILLY DHILLY na ZERE LA MAPOZI a.k.a MCHAFUZY watakuwa ndani ya Radio Kaya wakihojiwa live .Kupitia mahojiano hayo utaweza kujua mengi kuwahusu vichwa hawa wawili wa KILIFONIA CITY.Usikose kutegea hapo kesho.!
Friday, 3 May 2019
SWANYO BOY KAFUNIKA SHESHE. !!

Star huyu anayegonga MOMBASA kwa sasa kwa jina SWANYO BOY kafunika hapo DANS LOUNGE jana usiku kama tunavyopokea habari toka meza yetu.Msanii huyo aliyeambatana na manager wake pia ameambatana na msanii HALF DOZE aliyewika na track BOM BOM aliyofanya na SUSUMILA miaka ya nyuma.
Kwa kweli mafans wameinuka alipopanda SWANYO BOY stejini.Msanii huyo amefanya warembo wapandwe na mzuka alipoachilia nyimbo yake kali BOUNTY KILLER.Kwa kweli kulikuwa na wasanii wengi walioperform lakini SWANYO BOY amefunika shoo.Big up sana SWANYO BOY@Nuktasaba
Thursday, 2 May 2019
DOUBLE MIND ANAKUJA VIZURI
Msanii anayefahamika kwa jina DOUBLE MIND anakuja vizuri sana kwenye game ya muziki.Msanii huyu wa MOZTACH RECORDS anazidi kutisha na Track aliyoifanya hivi majuzi inayofahamika kama UCHI UCHI.DOUBLE MIND ameiambia meza yetu ataiachilia muda wowote toka saa hii ikiwa na video yake .Mzuka huo alioufunika jana kwenye shoo ya DABASO WARD FOOTALL LEAGUE FINAL ilimfanya hadi MCA wa eneo hilo MH.EMMANUEL CHANGAWA ajitoe kwenye kiti apande stejini ajirushe..
Kwa kweli hii ilidhihirisha ukali wa ngoma hiyo.Track hiyo iliinua hadi wasanii wengine wa MOZTACH ikiwemo TRILLY,SEEFAR na TMATSI .Nyimbo hiyo ikidondoshwa utaipata hapa Nuktasaba.Usikae mbali.
Tuesday, 30 April 2019
SWANYOBOY KUKINUKISHA @DAN'S LOUNGE
Monday, 29 April 2019
MSANII MEDALLION APATA AJALI
Msanii mkali na pia mshindi wa tuzo za Kilifi Got Talent,Medallion ahusika katika ajali ya barabarani.Muimbaji huyo,kulingana na habari zilizofikia meza yetu ni kwamba alikuwa ametoka kupiga show mjini Watamu mnamo siku ya Jumapili tarehe 28 na alikuwa katika harakati za kurudi nyumbani.Baada ya kupiga show Watamu ,Medallion aliabiri pikipiki ili kufikishwa Gede ambapo angepata usafiri wa kumfikisha Kilifi kwenye makaazi yake.
Ajali hiyo imeripotiwa kutokea maeneo ya Gede wakati dereva wa pikipiki aliyokuwa ameabiri msanii huyo aliposhindwa kudhibiti mwendo alipofika kwenye tuta (bump) .Akiambatana na Medallion alikuwa msanii mwenza Fikreen Mafito ambaye alikuwa ameabiri pikipiki nyengine.Msanii Medallion aliharakishwa zahanati ya Gede ambapo baada ya kupata huduma ya kwanza msanii huyo alipelekwa katika hospitali ya rufaa mjini Kilifi.Wasanii ambao wameweza kufika hospitalini humo kumjulia hali ni pamoja na Producer wake Dhilly Dhilly,Crash V, Lemmy K na wengineo.NuktaSaba inamtakia Medallion afueni ya haraka ikikumbukwa pia Msanii wa Hip Hop kutoka Pwani ya Kenya, Malindi, Fash P pia anaendelea kuuguza majeraha baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani pia.Tunawaombea afueni ya haraka wasanii wetu!

KINAYA CHA STARDUST MALINDI
Msanii mkongwe wa mziki wa aina ya Kaya HipHop mjini Malindi,Mitaa Kisauni adhihirisha kutoridhishwa kwake na mipangilio ya burudani ya ukumbi wa Stardust mjini humo.Mitaa amezungumzia haya baada ya kuona mabango mengi ya wasanii wa nyumbani kuwa wanapewa nafasi za kutumbuiza mahali hapo .Kuna wasanii kama vile Shabigy,Angie Fresh,Dotty Shuqx,Dogo Richie na wengine wengi ambao wengine wameshafanya kazi zao hapo ilhali wengine wakiwa wameratibiwa kutumbuiza pia.
Kulingana na Mitaa, anasema Stardust imekuwa na historia ya kuwapa shows wanamziki wa nyumbani wakati wa kusi ,muda unaoaminiwa na wengi kuwa pesa hupotea na biashara huwa chini sana.Ingekuwa kweli viongozi wa Stardust wanasapoti talanta za nyumbani na kuwa na moyo wa kuwaendeleza wasanii wakizingatia kuwa sanaa ni ajira basi wangekuwa wanawapa wasanii hawa shows kuanzia mwezi wa nane mpaka mwezi wa kumi na mbili wakati huwa season iko juu na pesa ipo lakini utakuta show za wasanii wa nyumbani nyingi huwa ni kuanzia mwezi wa tatu,wa nne mpaka mwezi wa sita hapo ambapo huwa pesa hakuna.Msanii anapiga show na hakuna chochote anapata, season ikiwa sawa, show wanazipatia wasanii wa mataifa ya nje .Inakera sana!,asema Mitaa kwa uchungu. Ipo haja ya kubadilisha hali halisi ya burudani Malindi ili wasanii waweze kupiga hatua mziki kama ajira.

Sunday, 28 April 2019
Subscribe to:
Posts (Atom)