Staa wa RNB kutokea Pwani nchini Kenya kawahi dili ya utangazaji kwenye stesheni ya radio ndani ya county 002.Radio stesheni anayofanyia staa huyu inafahamika kwa jina RADIO KAYA iliyoko KWALE .Alipoulizwa na meza yetu kuhusu utenda kazi wake amefunguka hivi,
"Kipindi changu ni DZILONI MBIDZO kuanzia saa kumi jioni hadi saa moja usiku (4pm-7pm) kila jumatatu hadi ijumaa,narusha mangoma na salamu kwa lugha ya kimijikenda ikiwa LENGO ni Kuhakikisha kwamba wa mijikenda na wakaazi wote wa pwani wanaitambua radio kaya kama redio ya kipekee na bora na pia kuinua vipaji vya watu wa pwani kupitia radio ikishirikiana na chama cha KILIFI COUNTY TALENT ASSOCIATION(KICOTA)".
Kwa kweli kipindi hiki kinabamba sana mashabiki kwa sababu MR BADO anaendelea kufanya vizuri na kibao chake kinachotamba kwa sasa kinachoitwa TETEMA style ya Mwanzele.
Tunamuombea mafanikio MR BADO .Usikose kusikiza RADIO KAYA 93.1FM MOMBASA,99.7 FM MALINDI#KITOVU CHA UMOJA WA PWANI.HAPA NDO NYUMBANI.
No comments:
Post a Comment