Thursday, 9 May 2019

PILI PILI FM YAGEUZWA KUWA ASENA FM

Stesheni ya radio iliyokuwa ikifahamika kama PILIPILI FM sasa iligeuzwa na inajulikana kama ASENA FM kama tunavyopata habari kutoka kwa ripota wetu.Radio hiyo iliyopatikana kwenye mitabendi ya 92.5 fm Malindi ilikuwa inatememesha stesheni zote ndani ya County 001 kwa vipindi na watangazaji wakali wa kazi waliokuwa wakirusha burudani kwa mashabiki.PILIPILI ilikuwa na watangazaji waliomwaga moto walipokuwa kazini kama vile ERIC GATES MGENGE aliyewakilisha ndani ya kipindi MWAKE MWAKE.Kwa kweli mashabiki watawamiss watangazaji waliofanya kazi PILIPILI FM kwa sababu ASENA FM ilichukua crew mpya ya watangazaji kutoka radio nyengine hapa pwani.Kulingana na habari tulizopata huenda Radio hiyo iliuziwa Bwenyenye mwengine ambaye hatimaye aliamua kugeuze jina liwe ASENA FM na achukue kikosi kipya aanze nacho.Kitu tunachosoma pia kutoka kwa uamuzi huo,stesheni hii huenda itakuwa stesheni ya kimijikenda.Radio hiyo haijaanza kupeperusha vipindi kwa sasa lakini kuna ishara kwamba huenda ikaanza rasmi muda wote kuanza saa hii.
Radio hiyo ina watangazaji maarufu waliobobea kwa kazi za kijanja kama vile SISTA SHANNIEZ atakayekuwa na kipindi kiitwacho TAKE OVER ambapo atarusha ngoma na kuinua vipaji vya wasanii wa nyumbani.Mapresenter wengine watakaopeperusha vipindi moto ASENA Fm ni TEDDY NAYE,PUKAPYU, MEDZA MWANGEMI, FATUMA MWANGALA,IAN MGALLA,HENRY AMANI na wengineo.Kwa kweli stesheni hii huenda ikapagawisha mashabiki kwa sababu mapresenter wake wengi wamefanya kazi kwenye stesheni nyingine kubwa hapa pwani kama vile PWANI FM,BAHARI FM ,na KAYA FM. Tunaiombea ASENA FM mafanikio huku tukiitegea .

1 comment: