Thursday, 11 April 2019

HATIMA YA NUFACE FAMILY

NuFACE ni kikundi cha wanahiphop kutoka pwani ya Kenya. Ni kikosi kilichojumulisha wasanii kama J2 ,Rama Q na MB ZO. Kazi zao nyingi za kimziki zilifanywa chini ya uongozi wa Crack Sound Records mjini Kilifi inayomilikiwa na Jay Crack.Katika pekuzi za NUKTASABA mtandaoni,tulipatana na picha kadhaa zinazomuonyesha mmoja kati ya vichwa katika kundi hilo akiwa katika ulimwengu wa Jamaica kihisia na fikra. Wenyewe huita meditation.


NUKTASABA imeamua kumuangazia Msanii J2 ambaye alionekana kuwa kichwa na kiongozi wa kikosi hiki cha burudani.Walivuma na vibao kadhaa lakini PRETENDER ni kibao chao kilichotia fora zaidi.Je ,ni kweli msanii J2 anapanga kwenda katika vituo vya kurekebisha tabia hususani uraibu yaani rehab?


Kuna tetesi hizo kwamba J2 huenda hivi karibuni akapelekwa rehab ili kuokoa kipaji kilichoko ndani yake.Tulijaribu kumtafuta J2 kwa njia ya simu ili kudhibitisha hili ila juhudi zetu hazikufua dafu.Tunaendelea kufuatilia tetesi hizi,usisahau hapa ndipo chimbuko la 411 za mastaa wetu ndani ya Kaunti ya Kilifi .Usicheze mbali!

No comments:

Post a Comment