Wednesday, 25 April 2018

MSANII WA SIKU


Huu ni wakati wa kumjua msanii wa siku ya leo kama tunavyozipata habari kutoka kwa ripota wa kitengo hicho.Leo tuna msanii anayetambulika kama SEE FAR AKA SIFA SYMON .Msanii huyu ni mtu alianza mbali sana kwenye hii sanaa kitu kinachomfanya kuwa maarufu kwa haraka na kuwa makini kwenye utunzi wa vibao vinavoyumbisha anga za mziki kila vinapoachiliwa.Alihojiwa na ripota wetu na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo..

A.k... Vipi mkali.?

See Far: Nko shwari mwana.

A.k...:   Ulianza lini mziki ?

See Far  :Nilianza 2016 na kufanya ngoma studio ya Bianca ē Nero chini ya mkono wa Producer  Lameck Boy.Nyimbo hii iliitwa Sumu niliyomshirikisha UB DADDY na SIS KAY.Ilifanya vizuri kwa maredio ikashika chati kwa muda stesheni za pwani.

A.k.: Kwa nini ulikimya baada ya nyimbo hiyo kufanya vizuri ?

See  Far: Nilipata safari ya ghafla ya kikazi so ikanibidi nishikike kwa muda mrefu but saa hii nmerudi niko full ,Niko skopa ,niko ready kuachilia mapini hit baada ya hit .

A.k..Ok..sasa umerudi kwa game unafanya na studio gani ? Funguka...

See Far...MozTach Records na Producer Moses a.k.a MOZTACH mkali wa mabeat na michapo.Hata saa hii kuna ngoma mbili ziko jikoni -amore na ni wewe..Zote naamini zikitoka zitayumbisha anga za pwani na Kenya yote  .Napanga nifanye video ya ni wewe kufikia may ili niachilie pamoja na audio yake.Nataka nitetemeshe anga za pwani na Kenya yote kwa jumla..

A.k...Safi sana.Sasa unawambiaje mafans wako ?

See Far. .Najiamini nifanyacho so nawambia nawaundia mapini yenye yatawagonga vichwa na  yatawaacha hoi na kuwabamba kinyama.Kingine naomba sapoti yao mitandaoni coz kazi huzipost huko..

A.k..Morale sana kichaa wangu wa nguvu.Nakuombea mafanikio katika safari yako.

See Far...Pamoja.
A.k...Safi .

Hivyo ndo mahojiano yalivyoenda.Tunawaomba mafans nyote mufatilie habari mpya za sanaa hapa kwenye blog yetu..Enjoy !!..

No comments:

Post a Comment