Thursday, 26 April 2018
BARAKA DE PRINCE AZAMA WASAFI RECORDS PIA
Msanii mkali wa masauti kutoka Bongo Tanzania amezama tena Studio na kutoka na kitu kipya.Raundi hii amemshirikisha msanii anayekaa ulaya muda mwingi kwa jina la RJ
THE DJ na ngoma kwa jina "BORA IWE" .Ngoma hii mpya iliachiliwa jana ambapo inaendelea kupokelewa vizuri na mafans wao.Nyimbo hii imetengezwa na produsa mkali wa kazi LIZER kwenye Studio ya nguvu WASAFI RECORDS.Ngoma hii huenda ikaamsha ile tetesi iliyokuwa siku za nyuma kwamba THE PRINCE alikuwa yuko mbioni kutaka ku.sign mkataba na WCB .Mkali RJ THE DJ ni mtu atayeongeza soko la THE PRINCE sababu huwa shoo zake nyingi anazifanya majuu ikiwemo mitaa ya London na Uk kwa ujumla.Collabo hii pia itaongeza sifa zake apa East Africa sababu RJ huenda ana mipango ya kufanya kazi na wasanii wengine wa kambi ya WCB habari ambazo tunazifatilia na ripota wetu nyanjani.Endapo kuna ukweli wa THE PRINCE kufanya mkataba na WCB basi atakuwa ameweza hali ya kushika soko la East Africa kiumakini kama walivyoshika wakali wa WCB ikiwemo VANNY BOY NA HARMONIZE.Enyewe tunaiombea kazi i yao izidi kupokelewa vizuri na kushika mafans.Tunafatilia kazi tukiiwahi tutawadondoshea apa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment