Tuesday, 11 December 2018
10 DAYS BEACH FIESTA.....!!
Nuktasaba inakualika kwa Bonge la BEACH FIESTA itakayoanza tarehe 22/12/2018 hadi 01/01/2019 hapo SHELLY BEACH LIKONI-MOMBASA.Hili sheshe si la kukosa.Karibuni nyote.
PAT C x MEDALLION NA KITETE.
Wasanii wakali wa kili4nia PAT C na MEDALLION wanaachilia Bomba hapo kesho kwa jina KITETE.Ngoma hiyo huenda ikafanya vyema sababu itaachiliwa siku kubwa nchini KENYA yaani 12/12/2018 ikiwa watu wanasheherekea JAMHURI DAY na KITETE.Ikiachiliwa kesho utaidondoa hapa.
Friday, 5 October 2018
MEDALLION na DHILLY DHILLY KUPASUA TENA ANGA.!!
Wasanii wakali wa K TOWN wameamua kukinukisha tena.Wakali hao tunawaongelea Mkali wa masauti MEDALLION akiwa ubavuni na Mkongwe wa hizi kazi DHILLY DHILLY.Wakali hao wameiambia Nuktasaba Tarehe 5 0ctoba 2018 yaani leo wanaachilia bomba moto yaani NEW HIT kwa jina IVO IVO.Nyimbo hiyo iliyosubiriwa na mafans sasa iko tayari yaani inasubiri kulipua anga za burudani.Ukitaka kuisikia nyimbo hiyo ipate http://mdundo.com/song/1208018
Wednesday, 26 September 2018
SHABBIG AMEACHILIA KICHUPA KIPYA ..#AJAB SANA
Mkali wa vokolz yaani msanii bomba wa pwani na nchini KENYA kote ametimiza ahadi na mchapo wa kichupa alichokiachilia kwa mafans waliokisubiria kwa hamu.Mpini huo unaendelea kupasua vichwa na anga za burudani ni bonge la video ya nyimbo #AJAB SANA.Kwa kweli video inaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki kila kona na huenda ukanda ukaongeza soko lake msanii huyo kwa sababu imetayarishwa kwa u makini na ustadi sana.Tunamuombea mafanikio kwenye zake.Ukitaka kuitazama video ya AJAB SANA IPATE HAPA https://youtu.be/DJ5SXL8xxas
Thursday, 20 September 2018
SHABBIG KUDONDOSHA VIDEO MPYA
Msanii mkali kutoka pwani anataka kuachilia video ya ngoma ya AJAB SANA.Video hiyo iliyotayarishwa kwa ustadi sana tunaamini itagonga vichwa ndani ya pwani na Kenya yote kwa ujumla.Kwa kweli video hiyo ilisubiriwa kwa muda mrefu na mafans wa SHABBIG itawaacha hoi waionapo.Ukitaka kuipata idondoe https://youtu.be/_L3TIxZXZIM
Saturday, 8 September 2018
Wednesday, 5 September 2018
MSANII WA SIKU..!
Nuktasaba inakuletea msanii wa siku kama vile tulivyojulishwa na ripota wetu wa kitengo hicho.Msanii wa siku ya leo ni LANGE .Msanii huyu hujulikana pia na jina lake la kuongezewa kama LANGE MWEPESI.Msanii huyu anafanya muziki wake na studio kali ya CRACK SOUND RECORDS mjini KILIFONIA.Studio hii iko chini ya mkono wa Produsa hodari sana kwa mabeat na kazi safi kwa jina JAY CRACK.Kuna mengi usiyoyajua kuhusu LANGE MWEPESI ambayo leo utayafahamu.LANGE MWEPESI ni msanii kutoka kanda ya pwani .Alianza safari yake ya mziki toka akiwa kidato cha kwanza ambapo alitia mkazo pindi mashabiki wake walipomkubali ni mkali yaani anaweza kuelimisha na kuongoa hadhira kupitia kipaji chake .Kuna muda mashabiki wake walimuita LANGE A.K.A DAKTARI WA MISTARI ,yaani malenga stadi msumbufu balaa akamatapo MIC watu wanapagawa. LANGE MWEPESI alijulikana na track kwa jina "ADDICTION" ambayo ilifanya vizuri .Track hii ilitamba sana kwenye redio za pwani na kenya yote kwa ujumla. LANGE MWEPESI baadaye aliachia kibao chengine kilichoitwa"TUONANE".Kibao hicho alimshirikisha mkali wa sauti kutoka pwani SHA BBIGY.Kwa kweli mpini huo ulishika sana mashabiki.Kibao hicho kilichukua anga za pwani yaani kikatamba kwenye chati na mitandao.Pia LANGE alifanya ngoma na mkongwe wa hip hop kutoka pwani bado "MASTER KIMBO"ambayo ngoma hiyo ilikua kama cypher ila ilishika mashabiki.LANGE ashafanya kazi na kundi lifahamikalo Kama GALLANT PASASHA.Kundi hili lilfanikiwa kunyakua tuzo ya best collaboration song of the year ndani ya "KCPA awards" iliyoitwa "Ghetto Gal"Pia kuna video mpya inayotamba sana mitandaoni kwa jina MY LIFE ambayo iko kwa yutube channel ya GallantPasashaEmpire ambapo ukitaka unaweza kuidondosha hapa.Kundi hili linapanga kuachilia kibao kipya kwa jina COCO ifikapo tarehe kumi na tano huu mwezi wa tisa ambacho mtakipata hapa Nuktasaba kikiachiliwa.Kwa kweli LANGE ashafunika show club kadhaa ikiwemo BIBO LOUNGE,DANS LOUNGE kule Ukunda ikiwemo kumbi nyingine za burudani.Alipopewa fursa na ripota wetu afunge mahojiano alikuwa na haya ya kuongea "Kitu kizuri ambacho naweza kufunga nacho katika haya mahojiano ya moja kwa moja na nukta saba nikuwa,tukitaka kufika mbele sisi kama wasanii na tuwajibike zaidi pasi kuangalia favors sababu wapo wengi ambao uwezo wao balaa ila wanawekea wengine gundu ili kutofika mbele kimaendeleo,ila kwa uwezo wa maulana hakuna barabara ikakosa kona na imani tutashinda full. Nawapenda mashabiki wa pasasha nje na ndani ya sayarii hii ya 3.
CHENDA CHENDA 9-9 FESTIVAL.!!
Muungano wa wazee wa kaya za wamijikenda wanawaalika nyote kwenye sherehe kubwa ya kabila zote za kimijikenda siku ya JUMAPILI TAREHE 9-9-2018 utakaofanyika kwenye uwanja wa KARISA MAITHA hapa KILIFI.Viongozi wote wa pwani wanatarajiwa kuhudhuria.Usikose kufika uje usherehekee na ujivunie na wapwani wote.!
Tuesday, 4 September 2018
Friday, 31 August 2018
JE, NI KWELI KIKUNDI CHA YAKWETU KILIVUNJIKA?
YAKWETU ni kikundi cha vijana watatu wenye uwezo mkali hasa wa kuandika mashairi yenye mvuto na hisia.Vijana hawa akiwemo Supreme,Mike Planet na Matalanta pia wamebarikiwa na sauti na uwezo wa kuimba.Walipochipuka,watatu hawa waliweza kutuletea kibao OLELE kilichofanywa studio za Tempoz chini ya Producer Amz.Kibao hiki kiliwapa mashabiki wengi na umaarafu wakaupata baada ya ngoma hiyo kupata sapoti ya nguvu kutoka kwa stesheni kadhaa za kanda ya Pwani.Baadaye YAKWETU walirudi jumba lile lile Tempoz na kutuletea kibao SUGAR ambacho kilipeta zaidi ya OLELE.Baada ya muda mwingi wa kumiliki chati za Pwani na kibao chao cha SUGAR ,tetesi zikavuma kuwa kuna mzozo ndani ya muungano huo.Kumekuwa na kimya kirefu baada ya kibao SUGAR,jambo linalochangia kuleta ukweli wa tetesi hizi.
Kupitia mtandao wake wa Facebook,Mick Planet ameweka wazi kuwa amefanya colabo na msanii mwengine mbali na wenzake wawili.Ngoma hii inaitwa GARAMA ambayo inakuja pamoja na video yake hivi karibuni. Meza yetu ya dondoo za wanamziki ilijaribu kumtafuta Mick Planet ili kuthibitisha tetesi hizi,habari ambazo Planet amekanusha na kusema YAKWETU bado ipo na itazidi kuwepo."Ngoma na video ya Gharama kusema ukweli ipo,lakini hiyo ni colabo tu na wala haimaanishi YAKWETU imevunjika.Naamini kila mmoja wetu ana uwezo so deal inapotokea,haina budi kuchangamka",asema Planet.
Sisi letu ni kusubiri ili tuone kama watavunja kimya chao ama YAKWETU ndio ni basi! Pakua OLELE na SUGAR hapa
Wednesday, 29 August 2018
POPOTE KAMBI,CRACK SOUNDS YAHAMISHWA
Moja kati ya studio kali zaidi za mziki mkoani pwani, CRACK SOUNDS yapata makao mapya.Studio hii inayomilikiwa na Producer mkongwe JAY Crak,ni jumba ambalo limefanikisha kazi za wasanii tajika kanda ya pwani wakiwemo Shabig,Dhilly Dhilly,Fash P,Pat C,Master Kimbo,Kaa La Moto,Dogo Richie na wengine wengi.Crack Sounds ina historia ndefu ikizingatiwa ilipoanzia mpaka ilipofikia kwa sasa.Crack Sounds imefanikiiwa kuweza kupanua mbawa zake na kuwa na jumba sawia na lile lililoko mjini kilifi ambalo linahudumia wenye vipaji wa sehemu ya Mariakani na maeneo mengine ya karibu.Tawi la Crack Sounds Mariakani liko chini ya kakake wa damu Jay Crak anayefahamika kama Producer Lai.
Tunapozungumzia CRACK SOUNDS iliyoko katikati mwa jiji la Kilifi,tunazungumzia uti wa mziki katika County nzima ya Kilifi.Hivi majuzi studio hii iliweza kuhamishwa na kupelekwa sehemu mpya mtaa tofauti na ilipokuwa zamani.Walioijua CRACK SOUNDS ilipokuwa mwanzoni mwa mwaka huu na miaka kadhaa iliyopita,hawatapinga kuwa ilikuwa ikipatikana karibu na benki ya Barclays karibu na hoteli kubwa ya kifahari Titanic.Kwa sasa Studio hiyo imehamishwa mpaka mtaa wa kwa Charo Wa Mae karibu na mkahawa unaojulikana kama Half London.Ukiwa na uhitaji wa kufika studio ukiwa mtaa huo wa Charo Wa Mae,usisite kumpigia simu Jay Crak kwa nambari +254725917081 .
Usikose kutembelea blog yetu ya NUKTA SABA kwa habari zinazokuhusu kama hizi.I thought you should know !
Tunapozungumzia CRACK SOUNDS iliyoko katikati mwa jiji la Kilifi,tunazungumzia uti wa mziki katika County nzima ya Kilifi.Hivi majuzi studio hii iliweza kuhamishwa na kupelekwa sehemu mpya mtaa tofauti na ilipokuwa zamani.Walioijua CRACK SOUNDS ilipokuwa mwanzoni mwa mwaka huu na miaka kadhaa iliyopita,hawatapinga kuwa ilikuwa ikipatikana karibu na benki ya Barclays karibu na hoteli kubwa ya kifahari Titanic.Kwa sasa Studio hiyo imehamishwa mpaka mtaa wa kwa Charo Wa Mae karibu na mkahawa unaojulikana kama Half London.Ukiwa na uhitaji wa kufika studio ukiwa mtaa huo wa Charo Wa Mae,usisite kumpigia simu Jay Crak kwa nambari +254725917081 .
Usikose kutembelea blog yetu ya NUKTA SABA kwa habari zinazokuhusu kama hizi.I thought you should know !
Sunday, 26 August 2018
DHILLY DHILLY ATEKA ANGA TENA.
Msanii mkali kutoka kilifornia ameachilia tena mpini.Ngoma hiyo kwa jina MNACHOOMBA inaendelea kupokelewa vizuri na mafans wa pwani na kenya yote kwa ujumla .Hii kazi tunaamini itafanya vizuri sana anga zote za burudani.Tunamuombea mafanikio DHILLY DHILLY kwenye kazi yake.
Friday, 24 August 2018
MR BADO ARELEASE VIDEO MPYA
King wa RnB MR BADO aachilia video mpya .Video hiyo ina mtindo mkali wa kipwani ukiona itakuacha hoi.Ukitaka kuiiona ipate hapaMr.bado-Uthamu wa pwani 0fficial music video: https://youtu.be/W-ywANqT8GU
Sunday, 12 August 2018
Saturday, 11 August 2018
R.I.P KING MAJUTO@
Msanii mkali wa RNB toka pwani ameachilia kibao cha kumsindikiza mwenda zake KING MAJUTO.Kibao hicho amemushirikisha msanii mkali kwa jina VELVET aliyezidi kuongelea vyenye sanaa ya East Africa ilivyopata pengo na itakavyokosa mchango wake mcheshi huyo KING MAJUTO.Kwa kweli tutakukosa machoni ila hatutakusahau moyoni @R.I.P #KING MAJUTO..
Ukitaka kuipata nyimbo hiyo ipate hapa Mr.Bado ft Velvet(Rip king Majuto): https://youtu.be/ONjpcQ7_YJQ
Saturday, 4 August 2018
Monday, 9 July 2018
KISS CLAN WAMERUDI TENA NA MSHINDO.
Nuktasaba inakuletea habari za kundi la RNB linalojulikana kama KISS CLAN.Kundi hili lilianza mwaka wa 2000.Lilikuwa na wanachama watatu ikiwemo MR T, SHY LAVA na MZANYI MLUNJI.KISS CLAN walirekodi nyimbo ya kwanza FP REKORDS kwa jina MPENZI..Nyimbo ilipeta mtaani kwa muda wa miaka minne .Hizo enzi KISS CLAN walipata jina na kujulikana sana.Ilipofika 2006 kundi hilo lilienda Mombasa KAY REKORDZ na kifanya ngoma kwa jina USWAHILINI.Nyimbo hiyo ilifanya vizuri kwa maredio ikiwemo Pwani Fm.Baadaye kundi hilo lilienda GREEN HOUSE chini ya usimamizi wa produsa maarufu K SHORT likafanya nyimbo na NYOTA NDOGO iliyoitwa SINA .Track hiyo haikufanya vizuri sana.Walipata shoo klabu maarufu kama HAPPY NITE,COMEBACK WATAMU,LAMBARDA MTAWAPA ,STARDUST MALINDI na nyinginezo.KISS CLAN walifanya kazi na ma DJ maarufu kama DJ HUSSEIN,ALI PAPI na wengineo. Ilipofika 2007.KISS CLAN walifanya track iliyoitwa NAHUMANYANE.Kwa kweli track ilipendwa sana.Iliwainua sana KISS CLAN sababu ilitamba redio za pwani na kenya kwa ujumla ikiwemoK KBC,PWANI FM ,RADIO KAYA na nyinginezo.Soko la KISS CLAN likapanda sana kote nchiniv kwani track hii ilitumika kwenye maredio kuleta amani wakati wa mgogoro wa siasa na vita baada ya kura za 2007 nchini KENYA kwani NAHUMANYANE iliamanisha sote tujuane tusikosane tupendane.Kiss CLAN iliendelea kufanya vizuri sana.Nyimbo zao zilienea na kubamba kila mahali si maredioni si kwenye sehemu za burudani.Ilikuwa nyimbo zao zinajulikana na kila mtu kote kenya.KISS CLAN waliachilia track zengine bomba kama vile MIZANI ZA PWANI,WEEKEND NA PARTY zilizovuma pia.Ilipofika 2012 SHY LAVA alikuja pata na kifo cha ghafla bila sababu kitu kilicholeta mshtuko kwenye kundi hilo.Wawili waliobaki MR T na MZANYI MLUNJI waling`ang`ana wajua kiini cha kifo cha mwenzi wao lakini hawakufaulu.Hapo kundi likaanza kusambaratika mwisho likazima kabisa.Haikueleweka labda hawakuweza kukima malipo ya studio labda .Huo wakati kulikuwa na tetesi kwamba kundi hilo limepata promota anayetaka kuwapeleka Afrika kusini wakarekodi huko lakini hazikufua dafu ata walizidi kudidimia.Watu walifikiri huenda msanii mwenda zake ndiye aliyebeba nyota ya kundi hilo kung'ara labda.Yalisemwa mengi.Kufikia mwaka huu mwanzo MR T na MZANYI MLUNJI waliamua kurudi tena kwenye sanaa ata kufikia saa hii wana nyimbo mpya kwa jina NANI ATANISAIDIA wanayoipangia kuiachilia huu mwezi wa nane.Tunawaombea KISS CLAN mafanikio kwenye kazi yao
Tuesday, 26 June 2018
MR BADO @CLUB RED LION
Nuktasaba inakuarifu kwamba ifikapo jumamosi tarehe 30 Juni 2018 kutakuwa na bonge la tamasha la msanii kwa jina MR BADO A.K.A MZUNGU MGIRYAMA litalofanyika apo CLUB RED LION WATAMU.Kwenye sheshe kutakuwa na bonge la show ambapo MR BADO atatumbuiza mashabiki na muziki wa kitamaduni wa kimijikenda MWANZELE.Show hiyo itakuwa ya kukata na shoka kwani MR BADO ataburudisha watu LIVE hadi asubuhi.Hili sheshe si la kukosa kwani kiingilio itakuwa ni BURE.Nuktasaba inawaomba watu wote msikose kwani kutakuwa na fursa ya kuona LIVE vyenye muziki wa MWANZELE huwa unapigwa na kikosi cha MR BADO.
Hii si show ya kukosa uje upate utamu wa muziki wa kitamaduni hadi chee !!
KOSA UCHEKWE.!!!
Hii si show ya kukosa uje upate utamu wa muziki wa kitamaduni hadi chee !!
KOSA UCHEKWE.!!!
VIDEO IMEACHILIWA LEO !!
Nuktasaba inakujulisha kwamba FASH P leo ameachilia rasmi video ya nyimbo DEAR SON.Video hiyo iliyosubiriwa muda mrefu imedondoshwa leo na utaipata https://m.youtube.com/watch?v=z8Ytb5ckf1Yy
Friday, 22 June 2018
SHABBIG KUACHILIA NGOMA MPYA
Nuktasaba inakupa taarifa msanii mkali wa masauti kutoka kilifonia anayefahamika kwa jina SHABBIG anataka kuachilia ngoma mpya kwa jina AJAB SANA.Kibao hicho kimeundwa na ustadi sana na produsa mkali sana wa kuaminika .Mkali huyu aliyetingisha anga na kibao chake SHEMEJI alichoundiuwa na produsa AMZ amedai kazi hii mpya anaamini itazidi kupagawisha mafans wake zaidi kama alivyoambia ripota wetu wa Nuktasaba.SHABBIG kwa kweli huwa habahatishi na ameahidi ataendelea kuwapa mashabiki wake midundo moto moto hadi wapagawe yaani HIT baada ya HIT mwanzo mwisho.Kwa kweli SHABBIG ngoma zake huwa zinapasua anga za pwani yaani zinakubalika redio zote za pwani na mitandaoni hapa KENYA kila aziachiliapo.SHABBIG ameambia Nuktasaba kwamba bomba la AJAB SANA ataliachilia na video yake wakati wowote kuanza sasa so amedai mashabiki wawe tayari kuipokea.Nuktasaba na mafans wote tukae mkao wa kula tusubirie tindo hiyo iachiliwe na mkongwe huyo wa hizi kazi .Nuktasaba tunakuahidi kazi ikidondoshwa tutakupakulia hapa kwa blog yetu.So usiwe mbali !!
VIDEO MPYA IKO TAYARI KUACHILIWA
Msanii mkali wa HIPHOP toka pwani kwa jina FASH P the HOLLYSTAR ameiambia Nuktasaba kwamba video mpya ya DEAR SON iko tayari na ataachilia tarehe ishrini na sita huu mwezi wa sita 2018.Gwiji huyu mkali wa vina amedai kazi hiyo imetengezwa kwa ustadi sana na anaamini mafans wake wataikubali.Tunaisubiria video hiyo ikiachiliwa tu tutaiweka hapa kwa blog yetu uweze kuidondoa hapa.Tunamuombea mafanikio kwenye kazi zake.
Saturday, 16 June 2018
NEW VIDEO COMING SOON.@FASH P
Msanii mkali wa HIPHOP toka kaskazini ya Pwani kwa jina FASH P the HOLLY
IDD SPECIAL EXTENDED
MARIDHIA HOYEEEEEEE!!!!!!!!
DUE TO PUBLIC DEMAND UNGANA NA KUNDI ZIMA LA MARIDHIA SOUNDS SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17JUNE NDANI YA ZEITUNI BAR @BAMBURI
MPAKA CHEE....
NJOO TUENDELEE KUSHEREHEKEA IDD KIMARIDHIA......
KIINGILIO NI BUREEEEE!!!!!
KUFIKA KWAKO FURAHA KWETU.....```
*MARIDHIA SOUND, ILIURIDHIA MOYO WANGU.*
USIKOSE.!!!
DUE TO PUBLIC DEMAND UNGANA NA KUNDI ZIMA LA MARIDHIA SOUNDS SIKU YA JUMAPILI TAREHE 17JUNE NDANI YA ZEITUNI BAR @BAMBURI
MPAKA CHEE....
NJOO TUENDELEE KUSHEREHEKEA IDD KIMARIDHIA......
KIINGILIO NI BUREEEEE!!!!!
KUFIKA KWAKO FURAHA KWETU.....```
*MARIDHIA SOUND, ILIURIDHIA MOYO WANGU.*
USIKOSE.!!!
Sunday, 10 June 2018
Wednesday, 6 June 2018
Tuesday, 22 May 2018
Saturday, 19 May 2018
HARMONIZE AKOSOA WANAFIKI..!
Msanii mkali wa kambi ya WCB anayefahamika kwa jina HARMONIZE amewazima midomo wanafiki waliochonga ati uhusiano wake na Sarah unayumba na huenda ukavunjika karibuni kisa ni HARMONIZE alifumaniwa juzi na kidosho mwingine huko Dar es salaam mafichoni katika ukumbi fulani wa burudani.HARMONIZE amedai bado anampenda sana BABY wake SARAH na amepuzia uvumi wa kinafiki dhidi yake si wa ukweli kama alivyonukuliwa na ripota wetu anayefuatilia stori za mastaa kutoka WASAFI TV kule BONGO, TANZANIA.Ameongezea kuwa hata mipango yake ya kufunga ndoa na SARAH inaendelea vizuri ata huenda ndoa yao itimie ifikapo Disemba huu mwaka.Kwa kweli wanaolonga wamezimwa midomo yao.Ukitaka kupata habari mpya za wasanii tembelea blog yetu.
Friday, 18 May 2018
Friday, 11 May 2018
Tuesday, 8 May 2018
OFFICIAL LAUNCH
Ifikapo jumamosi tarehe kumi na mbili mwezi wa tano mwaka huu (12/5/2018) mashabiki wote wa MARIDHIA SOUNDS BAND wataelekea kule BAHARI BAR huko KILIFI ambako kutakuwa na uzinduzi rasmi wa BAND hiyo ukiongozwa na mwanzilishi wake MOZENGA .Pia kutakuwa na mgeni atakayeshirikiana na MOZENGA kufungua sheshe hilo rasmi bwana TUVA WEHU mubarikiwa wa masauti zakuvutia atakayetumbuiza mashabiki hadi wapagawe.Hapo kutakuwa na zegede litakalo burudisha mashabiki hadi chee kwani kikosi chote cha MARIDHIA ikiwemo KAY daktari wa Solo Guitar na kimehakikisha kitawatumbuiza mafans wote bila kipimo hadi chee.Kwa kweli hili si sheshe la kukosa .Sote tufike tukazuge na MARIDHIA SOUNDS BAND mpaka kuche.
KOSA UCHEKWE !!
WAKO WAPI..!!?
Mashabiki wa NuktaSaba wanaendelea kuuliza wako wapi MAJIZEE kundi la wakali wa RNB lililowika nchini Kenya mnamo mwaka wa 1996 hadi 2004.Kundi hili lilikuwa na wasanii watatu ikiwemo FLAVOUR POLLE, KUL CHARLY na GEOMU aka GEORGE MUWANGA raia wa nchi jirani ya UGANDA.Baadhi ya vibao vilivyonoga ni kama BABY TALK TO ME, WATU WOTE, NZOONI na NAKUPENDA vikiwemo vibao vyengine.Kundi hili lilifanikiwa kufanya show ya kumbukumbu ya janga la BOMB BLAST kwa jina PAMOJA 1999 lililofanyika hapo US EMBASSY jijini Nairobi .Hakika kundi hili lilinoga sana kwa sababu waliwahi hata kufanya show pamoja na marehemu BRENDA FASSIE hapo CARNIVORE GROUNDS,Nairobi na pia MAMBA DISCOTHEQUE,Mombasa ikiwa chini ya usimamizi wa SCHIMDBERG raia wa Uingereza.MAJIZEE pia walihawi kufanya kazi na kampuni mbali mbali ikiwemo ya vinywaji ya REDBULL iliyomilikiwa na SCHIMDBERG kitu kilichowapa umaarufu hata kugeuzwa jina kuitwa REDBULL BOYS na mbabe huyo.Walifanya show club nyingi nchini katika towns kama vile Thika, Nyeri, Nakuru, Eldoret, Kisumu, Machakos, na kwengine.Ilipofika mwaka wa 2002 umaarufu wa kundi hilo ulianza kwenda chini .Hapo ndipo msanii GEOMU alipokumbwa na hitilafu ya akili iliyomfanya aregeshwe kwao nchini UGANDA akashuhulikiwe kimatibabu hali iliyobidi apelekwe SOUTH AFRICA kwa utafiti zaidi. FLAVOUR POLLE na KUL CHARLY walirudi watamu ambako walienda kuendeleza kazi yao kama ma Dj katika klabu ya HAPPY NIGHT kitu ilowawezesha kufungua Studio ya mziki ya FP RECORDS.Hapa walifanya nyimbo kama DEDEDE, UTAWEZA na NATAKA MANZI wakishirikiana na kundi la RUFF TOUCH.Nyimbo hizi zilitamba sana wakati huo.FLAVOUR aliivuka boda hadi BONGO TANZANIA alikofanya kibao kwa jina SEMENI kilichotawala anga za KENYA na BONGO hasa alipofanya Semeni remix na mkali wa Rap SOLO THANG. Aliporudi nchini FLAVOUR hakukaa sana na studio aliiacha chini ya usimamizi wa PRODUCER ERICK aka R KUL na KUL CHARLY . Hatimaye yeye akaenda ITALY kikazi.Aliishi ITALY kwa muda lakini akarudi nchini baada ya miaka mitano na ujuzi wa Audio and sound Engineering .Toka hapo FLAVOUR hajaachilia ngoma nyengine kwa muda sasa .KUL CHARLY pia amekimya sana na hajafaulu kurudi kwa game kama enzi hizo.Team Nuktasaba tunawatafuta MAJIZEE waliko waeleze mafans wao walikojificha.
#WAKOWAPI ??
Monday, 7 May 2018
SHEHEREKEA BIRTHDAY NA CELEB
Huu ni wakati wa kuwatakia wale mashabiki wanaosherekea leo siku ya kuzaliwa" HAPPY BIRTHDAY "Maisha marefu na Muwe na Mafanikio katika maisha yenu.Leo kuna maceleb unaosheherekea nao ikiwemo ENRIQUE IGLEASIS msanii ambaye amefanya vizuri kwenye POP na alizaliwa kule Madrid Uhispania siku kama leo.Amefikisha 43 years.Nuktasaba inawatakia " A HAPPY BIRTHDAY AND LONG LIFE"
Sunday, 6 May 2018
MR BADO ADONDOSHA TENA MZUKA ......!
MR BADO ameachilia video ya nyimbo mpya kwa jina "ONA DADA"
Hakika amezima wanafiki midomo sababu ni takribani wiki mbili tangu aachilie video ya nyimbo "ULINGO" na saa hii amerudi tena ! Nyimbo hii mpya huenda ikafanya vizuri zaidi sababu inaendelea kupokelewa vizuri na mashabiki wake.Mfalme huyo wa RnB pwani ameahidi raundi hii hatalegeza mkono kwenye kazi yaani ataendelea kudondosha ngoma kali moja baada ya nyingine hadi mwaka uishe kama alivyonukuliwa na ripota wetu.Kwa kweli hii itamuinua sana kwa mashabiki wake na pia itaongeza soko la muziki wake hapa Kenya na ulimwengu wote kwa jumla.Alipoulizwa kuhusu tetesi za kwenda Bongo huu mwezi kufanya kazi zake huko alikuwa na usemi huu " Nmepanga naenda leo BONGO TANZANIA kwenda fanya video ya nyimbo EASY GO niliyomshirikisha PROFESSA JAY na pia nilikuwa nimeongea na MR BLUE ambaye ameningoja kwa muda nikamalize ile collabo na yeye nyimbo tuliyoanza kuirekodi mwaka jana kwenye studio fulani TANZANIA.Pia nina mipango na ALI KIBA dingi wa ROCKSTAR ambaye tulikuwa tumeongea akitaka nifanye naye collabo alafu ikiwezekana tufanye mkataba wa kubaki na ROCKSTAR lakini hayo mtayajua nikifika huko ". Kwa kweli MR BADO huenda akafika mbali kwenye muziki.Tunamuombea mafanikio MR BADO kwenye kazi yake.Ukitaka kupata video hiyo dondoa https://youtu.be/Y2sInmdhi3Y
Saturday, 5 May 2018
MOZENGA MOSS KUHOJIWA LIVE.!!@RADIO KAYA
Nuktasaba inafurahia kukufahamisha kwamba ifikapo kesho jumapili tarehe sita mwezi wa tano mwaka huu (06-05-2018) msanii mkali wa nyimbo za Bango kwa jina MOZENGA MOSS atakuwa hapo RADIO KAYA akihojiwa LIVE kwenye kipindi cha misakato ya bango.Apo tutaweza kujua mengi kumhusu.Pia tutajua vyema kuhusu kwa nini alifikiria kuanzisha band mpya ya MARIDHIA SOUND BAND.MOZENGA MOSS atatufahamisha line-up yote ya wapiga vyombo wakali wa band iyo ikiwemo yeye mwenyewe akiwa anawakilisha hapo kwa keyboard na tunes kali zinazowapagawisha ma addicts wa bango wazisikiapo. Atatueleza jinsi band hii alivyoipangia ili iweze kuteka anga za Pwani na Kenya kwa jumla kuleta burudani kwa mashabiki wote wa bango .Atazidi kufunguka jinsi band hiyo itakavyoweza kufikiwa na mashabiki wakiihitaji kwenye maharusi,kwenye party na kumbi nyingine mashabiki watakapokuwa wanataka burudani hiyo.Kwa kweli MOZENGA MOSS ameahidi atakuwa wazi na mipango yote kabambe itakayofanikisha MARIDHIA SOUND BAND kutoa burudani moto wa kuotea mbali kwa mafans wote yaani MARIDHIA ADDICTS
Tunawaomba mashabiki wote wasikose kusikiza mahojiano hayo kesho Live.!!
Friday, 4 May 2018
MSANII WA SIKU
Leo katika kitengo chetu cha Msanii Wa Siku tunamuangazia IBU BWAY.Ibu ni msanii kutoka kanda ya Pwani kaskazini mwa Kenya.Ni msanii mwenye talanta ya utunzi na pia uwezo mkubwa wa sauti.Alianza mziki mwaka wa 2013 na kufikia sasa amefanikiwa kurekodi ngoma tano zikiwemo Hello,Keketwa ambayo alishirikishwa na Kacharo,Umeniacha ambayo alishirikishwa na Seyyid,Wewe ambayo alifanya na Man Tiger ndani ya jumba la kukuza vipaji la MOZTACH RECORDS chini ya Producer mkali Moses Kingi almaarufu MOZ.
Hivi majuzi IBU alitoa ngoma mpya ONE AND ONLY ambayo kwa sasa inapeta sana katika anga za maredio na pia mitandao.Mashabiki wanaendelea kumpa sapoti baada ya kutoa video ya kibao hicho ONE AND ONLY.Video hiyo imepikwa ndani ya IMAGINE STUDIOS na kwa uhakika ni kazi iliyosheheni mapishi bora.Wale wapenzi wa mziki wa IBU BWAY wanaruhusiwa kupakua kazi wanazozipenda hapa na pia kutazama video ya ONE AND ONLY ni bure na rahisi katika mtandao wetu wa NUKTA SABA ambapo tunakuza vipaji na kulea talanta za ukweli.Tazama video hiyo hapa
Thursday, 3 May 2018
UCHAMBUZI WA MSANII.
Sasa imefikia wakati wa kufanya uchambuzi wa msanii kama tunavyozipata habari kutoka kwa ripota wetu wa kitengo hicho.
Celine Dion ni mmoja kati ya wasanii wakubwa na
wenye heshima kubwa sana duniani. Mpaka sasa
ana umri wa miaka 49 akiwa ni raia wa nchi ya
Canada.
Celine Dion ni miongoni mwa wasanii matajiri
duniani akiwa na utajiri wa dola milioni 630. Tangu
ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 12,
Celine Dion amefanikiwa kupata tuzo 300 kati ya
tuzo 400 alizowahi kushiriki.
Mpaka sasa Celine Dion amefanikiwa kuachia
nyimbo zisizopungua 378, kati ya hizo amefanikiwa
kuimba kwa kutumia lugha za nchi tofauti kama
vile; Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kijerumani,
Kiitaliano, Kilatini na Kijapani.
Uwezo wake wa kuimba kwa kupanda hadi kugusa
key ya mwisho ndiyo umewavutia watu wengi na
kumfanya kuwa maarufu zaidi duniani. Kutokana na
rekodi aliyoiweka Celine Dion na uwezo aliokuwa
nao hakuna msanii kutoka nchini Marekani ambaye
ameweza kuikaribia rekodi yake.
Ukitaka kupata habari mpya za wasanii tembelea blog yetu...
Leo tutamchambua msanii mkali
wa marekani kwa jina CELINE DION.Celine Dion ni mmoja kati ya wasanii wakubwa na
wenye heshima kubwa sana duniani. Mpaka sasa
ana umri wa miaka 49 akiwa ni raia wa nchi ya
Canada.
Celine Dion ni miongoni mwa wasanii matajiri
duniani akiwa na utajiri wa dola milioni 630. Tangu
ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 12,
Celine Dion amefanikiwa kupata tuzo 300 kati ya
tuzo 400 alizowahi kushiriki.
Mpaka sasa Celine Dion amefanikiwa kuachia
nyimbo zisizopungua 378, kati ya hizo amefanikiwa
kuimba kwa kutumia lugha za nchi tofauti kama
vile; Kiingereza, Kichina, Kifaransa, Kijerumani,
Kiitaliano, Kilatini na Kijapani.
Uwezo wake wa kuimba kwa kupanda hadi kugusa
key ya mwisho ndiyo umewavutia watu wengi na
kumfanya kuwa maarufu zaidi duniani. Kutokana na
rekodi aliyoiweka Celine Dion na uwezo aliokuwa
nao hakuna msanii kutoka nchini Marekani ambaye
ameweza kuikaribia rekodi yake.
Ukitaka kupata habari mpya za wasanii tembelea blog yetu...
Wednesday, 2 May 2018
MSANII WA SIKU
Msanii wa siku ya leo ni Justin Bieber .
Justin Bieber ni miongoni kati ya wasanii waliopata
umaarufu wakiwa na umri mdogo. Mpaka sasa
Bieber ana umri wa miaka 22 lakini ameshafanikiwa
kufanya mambo mengi kwenye industry ya muziki
ambayo inamfanya awemaarufu dunia nzima.
Pia Bieber amefanikiwa kupata tuzo kibao zikiwemo
za Billboard Music Award, Grammy Award, MTV
European Music Award na nyingine nyingi.
Bieber amefanikiwa kuachia albamu nne mpaka
sasa, ‘My World 2.0’ mwaka 2009, ‘Under The
Mistletoe’ mwaka 2011, ‘Believe’ mwaka 2012 na
‘Purpose’ Novemba 2015. Albumu yake ya nne
ilifanikiwa kuuza kopi milioni 44.7 kwa nchi ya
Marekani na iliuza kopi milioni 75 kwa dunia nzima,
pia imefanikiwa kuingia kwenye list ya kuwa ni mwa
albumu zilizouza kopi nyingi duniani.
Justin Bierber amefanikiwa kuingia kwenye top ten
ya Forbes Magazine kwa mara tatu mfululizo kama
‘Most Powerful Celebrities’. Pia amewahi kuwa
msanii wa kwanza video yake kupata views bilioni
kumi kwenye Vevo.
Japo amekuwa ni msanii mwenye vituko vingi kwa
kipindi cha nyuma na kupelekea kuachana na
mpenzi wake, Selena Gomez ilionekana kuwa
ulikuwa ni utoto lakini kwa sasa ameonekana
amebadilika kuja kwa vingine akianzia kwenye
wimbo wake wa ‘Sorry’ uliofanikiwa kupata views
zaidi ya bilioni moja na milioni 218 na bado
anaendelea kufanya vizuri.
Justin Bieber ni miongoni kati ya wasanii waliopata
umaarufu wakiwa na umri mdogo. Mpaka sasa
Bieber ana umri wa miaka 22 lakini ameshafanikiwa
kufanya mambo mengi kwenye industry ya muziki
ambayo inamfanya awemaarufu dunia nzima.
Pia Bieber amefanikiwa kupata tuzo kibao zikiwemo
za Billboard Music Award, Grammy Award, MTV
European Music Award na nyingine nyingi.
Bieber amefanikiwa kuachia albamu nne mpaka
sasa, ‘My World 2.0’ mwaka 2009, ‘Under The
Mistletoe’ mwaka 2011, ‘Believe’ mwaka 2012 na
‘Purpose’ Novemba 2015. Albumu yake ya nne
ilifanikiwa kuuza kopi milioni 44.7 kwa nchi ya
Marekani na iliuza kopi milioni 75 kwa dunia nzima,
pia imefanikiwa kuingia kwenye list ya kuwa ni mwa
albumu zilizouza kopi nyingi duniani.
Justin Bierber amefanikiwa kuingia kwenye top ten
ya Forbes Magazine kwa mara tatu mfululizo kama
‘Most Powerful Celebrities’. Pia amewahi kuwa
msanii wa kwanza video yake kupata views bilioni
kumi kwenye Vevo.
Japo amekuwa ni msanii mwenye vituko vingi kwa
kipindi cha nyuma na kupelekea kuachana na
mpenzi wake, Selena Gomez ilionekana kuwa
ulikuwa ni utoto lakini kwa sasa ameonekana
amebadilika kuja kwa vingine akianzia kwenye
wimbo wake wa ‘Sorry’ uliofanikiwa kupata views
zaidi ya bilioni moja na milioni 218 na bado
anaendelea kufanya vizuri.
BEACH BOOGIE BASH
Allstar Entertainment wanakutangazia ifikapo jumamosi mchana tarehe tano mwezi wa tano huu mwaka (5/5/2018) sote watu wa KILIFI COUNTY twashikana mpaka Kilifi mazingira park.Tamasha hii itaanza saa nane mchane hadi saa kumi na mbili jioni.Mwanzo kiingilio ni bure ,pili kutakuwa na wasanii na wachekeshaji watakaotumbuiza na shoo za kukata na show,tatu kutakuwa na show ya mashindano ya kucheza na mshindi atanyakua elfu 10,000/= taslimu.Kwa hakika burudani itabamba sana hapo mazingara park.Tujitokeze kwa wingi tukapande miti huku tukitumbuizwa na wanasanaa maarufu..TUSIKOSE
Tuesday, 1 May 2018
MISS TOURISM KENYA @KILIFI COUNTY
Kutokana na ripota wetu wa kitengo cha sanaa tunazipata habari kwamba ifikapo usiku wa jumamosi tarehe tano mwezi wa tano mwaka huu (5-5-2018)watu wote wataelekea kule SUN N SAND BEACH HOTEL kwenda kuwatazama wale warembo wa KILIFI COUNTY wataokuwa wanapambana nani atakayeibuka na Ushindi wa MISS TOURISM KENYA- KILIFI COUNTY EDITION.Tamasha hii itanoga sana sababu kutakuwa na burudani kali itayowakilishwa na wasanii wakali wa pwani wakiongozwa na ALI B.Hapo atatingisha umati na midundo yake mikali ya kipwani.Pia kutakuwa na msanii maarufu kwa kuagiza na kulipa "PAPAH" atakayetumbuiza watu na shoo bab kubwa itakayowacha watu hoi jinsi itakavyofunika umati utakaokuwa ndani ya SUN N SAND.Mwisho msanii moto sana anayepeperusha bendera ya kina dada ,mkali sana CONFUSER atafunga ulingo.Bila shaka shoo itabamba sana yaani kutawaka moto ,kutachimbika aisee.! Kwa kweli shoo hii si ya kukosa ,Tukutane huko .!
UCHAMBUZI WA WASANII -DRAKE
NuktaSaba inafurahia kukuletea ukurasa wa uchambuzi wa wasanii wa majuu toka kwa ripota wetu.Leo tuko na msanii anayetambulika kama DRAKE.
DRAKE anafahamika zaidi kwenye
industry ya muziki duniani.
Ni raia wa nchi ya
Canada, lakini ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo,
muandaaji wa muziki na muigizaji pia.
Drake ambaye yupo chini ya lebo ya Young Money
Entertainment (YME) aliyosaini mwaka 2009,
inayomilikiwa na Lil Wayne.
Nyimbo yake ya ‘Best I Ever Had’ ilifanikiwa kushika
namba mbili kwenye list ya Billboard Hot 100 na
albumu yake ya ‘Thank Me Later’ ilifanikiwa kushika
namba moja kwenye Billboard 200.
Drake amefanikiwa kuchukua tuzo za Grammy, tuzo
3 za Juno Awards, tuzo sita za BET Awards.
Kutokana na uwezo wake amefanikiwa kushirikishwa
kwenye nyimbo kibao na wasanii wa kubwa kama
Jazz, Kanye West, Rihanna, Rick Rose na wengine
wengi.
Kutokana na uwezo wake kuandika nyimbo nzuri na
kipaji cha kuimba Hip Hop na RnB ndiyo unawavutia
watu wengi na kumfanya kuwa miongoni mwa
wasanii bora wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye
Subscribe to:
Posts (Atom)