Wednesday, 5 September 2018

MSANII WA SIKU..!

Nuktasaba inakuletea msanii wa siku kama vile tulivyojulishwa na ripota wetu wa kitengo hicho.Msanii wa siku ya leo ni LANGE .Msanii huyu hujulikana pia na jina lake la kuongezewa kama LANGE MWEPESI.Msanii huyu anafanya muziki wake na studio kali ya CRACK SOUND RECORDS mjini KILIFONIA.Studio hii iko chini ya mkono wa Produsa hodari sana kwa mabeat na kazi safi kwa jina JAY CRACK.Kuna mengi usiyoyajua kuhusu LANGE MWEPESI ambayo leo utayafahamu.LANGE MWEPESI ni msanii kutoka kanda ya pwani .Alianza safari yake ya mziki toka akiwa kidato cha kwanza ambapo alitia mkazo pindi mashabiki wake walipomkubali ni mkali yaani anaweza kuelimisha na kuongoa hadhira kupitia kipaji  chake .Kuna muda mashabiki wake walimuita LANGE A.K.A DAKTARI WA MISTARI ,yaani malenga stadi  msumbufu balaa akamatapo MIC watu wanapagawa. LANGE MWEPESI alijulikana na track kwa jina "ADDICTION" ambayo ilifanya vizuri .Track hii ilitamba sana kwenye redio za pwani na kenya yote kwa ujumla. LANGE MWEPESI baadaye aliachia kibao chengine kilichoitwa"TUONANE".Kibao hicho alimshirikisha mkali wa sauti kutoka pwani SHA BBIGY.Kwa kweli mpini huo ulishika sana mashabiki.Kibao hicho kilichukua anga za pwani yaani kikatamba kwenye chati na mitandao.Pia LANGE alifanya ngoma na mkongwe wa hip hop kutoka pwani bado "MASTER KIMBO"ambayo ngoma hiyo ilikua kama cypher ila ilishika mashabiki.LANGE ashafanya kazi na kundi lifahamikalo Kama GALLANT PASASHA.Kundi hili lilfanikiwa  kunyakua tuzo ya best collaboration song of the year ndani ya "KCPA awards" iliyoitwa "Ghetto Gal"Pia kuna video mpya inayotamba sana mitandaoni kwa jina MY LIFE ambayo iko kwa yutube channel ya GallantPasashaEmpire ambapo ukitaka unaweza kuidondosha hapa.Kundi hili linapanga kuachilia kibao kipya kwa jina COCO ifikapo tarehe kumi na tano huu mwezi wa tisa ambacho mtakipata hapa Nuktasaba kikiachiliwa.Kwa kweli LANGE ashafunika show club kadhaa ikiwemo BIBO LOUNGE,DANS LOUNGE kule Ukunda ikiwemo kumbi nyingine za burudani.Alipopewa fursa na ripota wetu afunge mahojiano alikuwa na haya ya kuongea "Kitu kizuri ambacho naweza kufunga nacho katika haya mahojiano ya moja kwa moja na nukta saba nikuwa,tukitaka kufika mbele sisi kama wasanii na tuwajibike zaidi  pasi kuangalia favors sababu wapo wengi ambao uwezo wao balaa ila wanawekea wengine gundu ili kutofika mbele kimaendeleo,ila kwa uwezo wa maulana hakuna barabara ikakosa kona na imani tutashinda full. Nawapenda mashabiki wa pasasha nje na ndani ya sayarii hii ya 3.

No comments:

Post a Comment