Friday, 31 August 2018

JE, NI KWELI KIKUNDI CHA YAKWETU KILIVUNJIKA?



YAKWETU ni kikundi cha vijana watatu wenye uwezo mkali hasa wa kuandika mashairi yenye mvuto na hisia.Vijana hawa akiwemo Supreme,Mike Planet na Matalanta pia wamebarikiwa na sauti na uwezo wa kuimba.Walipochipuka,watatu hawa waliweza kutuletea kibao OLELE kilichofanywa studio za Tempoz chini ya Producer Amz.Kibao hiki kiliwapa mashabiki wengi na umaarafu wakaupata baada ya ngoma hiyo kupata sapoti ya nguvu kutoka kwa stesheni kadhaa za kanda ya Pwani.Baadaye YAKWETU walirudi jumba lile lile Tempoz na kutuletea kibao SUGAR ambacho kilipeta zaidi ya OLELE.Baada ya muda mwingi wa kumiliki chati za Pwani na kibao chao cha SUGAR ,tetesi zikavuma kuwa kuna mzozo ndani ya muungano huo.Kumekuwa na kimya kirefu baada ya kibao SUGAR,jambo linalochangia kuleta ukweli wa tetesi hizi.

Kupitia mtandao wake wa Facebook,Mick Planet ameweka wazi kuwa amefanya colabo na msanii mwengine mbali na wenzake wawili.Ngoma hii inaitwa GARAMA ambayo inakuja pamoja na video yake hivi karibuni. Meza yetu ya dondoo za wanamziki ilijaribu kumtafuta Mick Planet ili kuthibitisha tetesi hizi,habari ambazo Planet amekanusha na kusema YAKWETU bado ipo na itazidi kuwepo."Ngoma na video ya Gharama kusema ukweli ipo,lakini hiyo ni colabo tu na wala haimaanishi YAKWETU imevunjika.Naamini kila mmoja wetu ana uwezo so deal inapotokea,haina budi kuchangamka",asema Planet.

Sisi letu ni kusubiri ili tuone kama watavunja kimya chao ama YAKWETU ndio ni basi! Pakua OLELE na SUGAR hapa

1 comment: