Monday, 9 July 2018

KISS CLAN WAMERUDI TENA NA MSHINDO.

Nuktasaba inakuletea  habari za kundi la RNB linalojulikana kama KISS CLAN.Kundi hili lilianza mwaka wa 2000.Lilikuwa na wanachama watatu ikiwemo  MR T, SHY LAVA na MZANYI MLUNJI.KISS CLAN walirekodi nyimbo ya kwanza FP REKORDS  kwa jina MPENZI..Nyimbo ilipeta mtaani kwa muda wa miaka minne .Hizo enzi KISS CLAN walipata jina na kujulikana sana.Ilipofika 2006 kundi hilo lilienda Mombasa KAY REKORDZ na kifanya ngoma kwa jina USWAHILINI.Nyimbo hiyo ilifanya vizuri kwa maredio ikiwemo Pwani Fm.Baadaye kundi hilo lilienda GREEN HOUSE chini ya usimamizi wa produsa maarufu K SHORT likafanya nyimbo na NYOTA NDOGO iliyoitwa SINA .Track hiyo haikufanya vizuri sana.Walipata shoo klabu maarufu kama HAPPY NITE,COMEBACK  WATAMU,LAMBARDA MTAWAPA ,STARDUST MALINDI na nyinginezo.KISS CLAN walifanya kazi na ma DJ maarufu kama DJ HUSSEIN,ALI PAPI na wengineo. Ilipofika 2007.KISS CLAN walifanya track iliyoitwa NAHUMANYANE.Kwa kweli track ilipendwa sana.Iliwainua sana KISS CLAN sababu ilitamba redio za pwani na kenya kwa ujumla ikiwemoK KBC,PWANI FM ,RADIO KAYA na nyinginezo.Soko la KISS CLAN likapanda sana kote nchiniv kwani track hii ilitumika kwenye maredio kuleta amani wakati wa mgogoro wa siasa na vita baada ya kura za 2007 nchini KENYA  kwani NAHUMANYANE iliamanisha sote tujuane tusikosane tupendane.Kiss CLAN iliendelea kufanya vizuri sana.Nyimbo zao zilienea na kubamba kila mahali si maredioni si kwenye sehemu za burudani.Ilikuwa nyimbo zao zinajulikana na kila mtu kote kenya.KISS CLAN waliachilia track zengine bomba kama vile MIZANI ZA PWANI,WEEKEND NA PARTY zilizovuma pia.Ilipofika 2012 SHY LAVA alikuja pata na kifo cha ghafla bila sababu kitu kilicholeta mshtuko kwenye kundi hilo.Wawili waliobaki MR T na MZANYI MLUNJI waling`ang`ana wajua kiini cha kifo cha mwenzi wao lakini hawakufaulu.Hapo kundi likaanza kusambaratika mwisho likazima kabisa.Haikueleweka labda hawakuweza kukima malipo ya studio labda .Huo wakati kulikuwa na tetesi kwamba kundi hilo limepata promota anayetaka kuwapeleka Afrika kusini wakarekodi huko lakini hazikufua dafu ata walizidi kudidimia.Watu walifikiri huenda msanii mwenda zake ndiye aliyebeba nyota ya kundi hilo kung'ara labda.Yalisemwa mengi.Kufikia mwaka huu mwanzo MR T na MZANYI MLUNJI waliamua kurudi tena kwenye sanaa ata kufikia saa hii wana nyimbo mpya kwa jina NANI ATANISAIDIA wanayoipangia kuiachilia huu mwezi wa nane.Tunawaombea KISS CLAN mafanikio kwenye kazi yao

No comments:

Post a Comment