Stage name yake ni ATUMIK WALEO.Yeye ni singer anayefanya muziki style ya Afro Pop.Alianza muziki mwaka wa 2015.Alifanya kazi zake kwenye studio iliyoitwa WAPISHI MUSIC RECORDS iliyoko Mtwapa chini ya produsa TINO.Alifanya nyimbo kadhaa ambazo hazikufika album yaani Mini Album .Nyimbo hizi zilikubalika na washikaji wake kwa sana.Alijaribu kuzipush ila hazikufaulu sana kuingia masikioni mwa mashabiki wengi so ikabidi asifaulu kutoka.Ilipofika 2018 ikambidi ageuze studio.Studio aliyohamia inafahamika kama ONE BLOOD PRODUCTION chini ya Produsa LIL I.Kwenye studio iliyopo Mtwapa amefanya kazi kama vile MAPENZI,USIENDE MBALI ,NAICHUKUA aliyomshirikisha Master Kimbo na zingine mob.Kufikia sasa amekamilisha albamu ambayo inamaliziwa kutayarishwa jikoni.Kufikia 2020 aliachilia nyimbo inayoitwa MADOIDO .Track hii imekubalika sana.Imekuwa club banger ,imetembea vizuri mitandaoni hata video yake imetrend sana.Itazame hapa.Kwa kweli jina la ATUMIK WALEO limekuwa gumzo kwenye maredio ambayo yanacheza muziki wake hapa pwani ikiwemo Msenangu fm,Pwani fm,Radio Jahazi,Kaya fm,Boss Radio na Baraka fm.Tulipomuuliza kuhusu changamoto anazopata amedai kutoa video kali ya kila nyimbo aachiliayo ndiyo ni ngumu kwake juu hajakuwa na mshiko wa heshima sana halafu pia baadhi ya maDj na mapresenters wa radio fulani hapa pwani huwa ni ngumu kufikiwa na muziki wake so hawawezi kuucheza.Amedai vitu hivi vinampa dharubu sana sababu yeye pia anatamani afike level ya kama masuperstar wengine wanavyokubalika kote ila bado.Ameongeza kwamba muziki wake unapatikana kwenye platform zifuatazo:-
Mdundo - Tembelea hapa
Youtube - Tembelea hapa
Mwisho ,ATUMIK WA LEO ameomba support kwa mashabiki wote wa Kilifi County na Kenya yote kwa jumla.Amedai "Albamu yangu ipo jikoni na nitaiachilia muda wowote kutoka saa hii so kuweni rada juu itakuwa moto sana yaani hatari fire".Kwa kweli msanii huyu ana uwezo mkubwa sana kwa hiyo tuendelee kumsaidia kusukuma kazi zake afike far.
#GoodLuck ATUMIK WALEO...
No comments:
Post a Comment