Sunday, 29 March 2020

TUJIEPUSHE NA CORONA#FARISY# MAUJANJA WAONYA !!


Nuktasaba leo imepata fursa ya kuongea na wasanii kadhaa kuhusu janga hili la CORONA.Msanii kutokea  G TOWN ambaye ni mwanaharakati anayetambulika kama MAUJANJA MASHBZO amefunguka na kuongea yafuatayo " Janga hili la CORONA limevamia KENYA na ni hatari  sana.Inafaa tufuatilie maelekezo ya serikali tunayopewa .Kwanza tuoshe mikono na sabuni kwenye maji safi ya kutiririka.Pili tusipeane mikono wala tusikumbatiane tunaposalimiana.Tatu tunapokohoa au kuchemua tujizibe na kitambara cha usafi au handkerchief".
Msanii wa pili anayeitwa FARISY EXPERT kutokea anga za WATAMU amekuwa na haya ya kusema "Ugonjwa huu wa COVID -19 umetetemesha dunia kwa sasa.Umeleta madhara makubwa sana hapa Kenya kwa hivyo itabidi tuwe makini sana tujiepushe.Kuna vitu kadhaa ambavyo natuzingatie ,kwanza tuambatane na maagizo ya serikali.Pili tujiepushe kushare vitu kama sigara,maji ya kunywa kwenye chupa moja.Tatu tuvae mask inayoziba pua na mdomo inayozuia kupata chembe chembe ya virusi vinapoachiliwa hewani endapo mtu amekohoa au kupiga chafya mnapokaribiana".
Ishara za Ugonjwa huu ni mwili kuwa moto, kikohozi kibichi,mtiririko wa makamasi,kichwa kuuma,uchovu wa mwili,koo kukauka na homa.
Kwa kweli janga hili limeathiri sana wengi na endapo mtu utajihisi una ishara za Ugonjwa huu fanya hima ufike kituo cha afya kilichokaribu nawe juu ukificha itakuua.Kwa hiyo tuwe makini tujilinde tuepuke kusambaa kwa  CORONA.Pia watu waache kudanganywa na habari potofu mitandaoni ya kwamba kunywa chai ya majani bila sukari ni dawa ya CORONA.Ni uongo.


#LetsFightCorona Now.

2 comments: