Msaniii anayefanya vizuri tokea bongo,Tz ambaye yuko nchini kwa sasa kwa ajili ya SHOW ambazo anafanya wikendi hii hapa nchini leo ametoboa jipu jinsi alivyofunguka.Staa huyo DULLY SYKES aliyekuwa Msenangu FM leo akihojiwa amefunguka na kudai kwamba wasanii wa Mombasa wanakosa sapoti kutoka kwa maPresenter wa Radio za Pwani na Ma Dj wa Pwani.Kwa kweli ameshtua presenter huyo na Dj waliokuwa wakimhoji.Ametoa mfano wa staa MASAUTI ,SUSUMILA na wengineo.Ameongezea ya kwamba "MASAUTI hangeenda NAIROBI angetegemea presenters na Ma Dj wa Mombasa angebaki Mombasa masauti yake". Na hii imewadhalilisha sana sababu imeonyesha sanaa hapa pwani watu hawapeani sapoti.Hii inaonyesha mapresenter wako radhi wacheze nyimbo za wasanii wa nje bure lakini za hapa mpaka wapewe kakitu ndiyo wacheze.Amesikitishwa kwa kutoa mfano kama wa kina KINGSTING na BEDBUG ambao walihit na ANISA miaka ya zamani ila hawajatoboa na mziki sababu walibaniwa.Hii inasikitisha sana.Inafaa kuwe na sapoti toka pande hizi ndiyo kimziki watu watafika far.Haina maana maDj na maPresenter wabanie wasanii ,inafaa iwasaidie ili watoke ndiyo wataona faida za sanaa yao.Jambo hili linafaa maDj na maPresenter walioko Mombasa,Kilifi,Malindi na kote Kenya watoe sapoti ili wakuze wasanii wao wafike far Sio Kuwabania.
No comments:
Post a Comment