Msanii kutoka 003 anayejulikana Kama NRICKY kahama kundi la Gmba Lord's Music.Hii ilifikia meza yetu alipoiambia anafanya kazi mpya kama project yake akimhusisha JAY GRAVITY msanii wa Nairobi na hakutaja GLM kwenye kazi hiyo.Mtu aliyemtaja kwenye track hii ni kakake anayefahamika Kama DOPE MASTER.Tulipomuuliza zaidi kuhusu DOPE MASTER amedai yeye ndiye promoter wa kazi hiyo hadi video atagharamia.Kwa KWELI msanii huyu ameshangaza wengi juu amelelewa na kukua na GLM.Haijabainika pengine ametaka kuwa Solo na kusukuma kazi zake pekee badala ya kundi.Pengine anamfuata aliyekuwa CEO wa GMBA LORDS MUSIC (GLM) kwa jina FASH P aliyedai amejitoa kundi hilo mwanzoni mwa 2019 ila anashangaza mashabiki sababu kazi zake bado zina nembo ya GLM.Kwa kweli Jambo hili limekithiri sana kwenye muziki wa Malindi kwa mfano ndani ya chocolate city kulikuwa na kundi la Ya Kwetu Band na MICK PLANET anafanya kazi kama Solo Artist,Fash P katoka GLM kuwa Solo,saa hii NRICKY pia !?
Mashabiki wanaanza kuamini kwamba kufanya muziki kama kundi huwa wasanii hawatoboi ndio anaenda SOLO .
No comments:
Post a Comment