Wednesday, 4 September 2019
COCO FEST IMEACHIA WASANII MACHUNGU#MALINDI
Coco Fest 2019 ni tamasha lililoandaliwa na Kibali Villas wakishirikiana na tourism ambassadors kupitia kwa mfuko wa serikali ya County ya Kilifi.Chakushangaza ni kwa nini wasanii waliotoka nje ya county hii kama vile NANDY,WILLY PAUL na,ERICK OMONDI walitumbuiza na kupokea malaki ya hela, pesa ambayo ni ya county ya Kilifi ilhali wasanii wa Kilifi County hawajalipwa ?Inauma sana sio poa!Wasanii wa Kilifi County walikuwepo ni kama vile KLEANHEART,CONFUSER J,MUZIQREBORN,JASLU,ANGIE FRESH,WADOSI BAND,FANISI BAND NA KATOI WA TABAKA.Chakustaajabisha ni kuwa tumekumbana na comment ya mmoja ya hawa wasanii hao mitandaoni bado akiulizia hela za malipo na baada ya kufuatilia ni kuwa asilimia 90 ya wasanii wa Kilifi county hawajalipwa chochote. Swali hili pia limeanikwa na mabloga kadha.Kufuatilia uchunguzi wetu umetuonyesha kuwa zoezi zima la tamasha hili lilikuwa mikononi mwa kibali villas wanaosemekana ambao kufikia saa hii imekua ngumu kuwasiliana nao ila bado tupo mbioni kutafuta usemi wa mmiliki wao bwana Paul Kimani.Tunamfuatilia mmiliki huyu atupe ukweli sababu sio vizuri wasanii wa nyumbani waachwe mataani bila hela wageni ndiyo wafaidi.Jambo hili limekera wasanii wa Malindi na County 003 yote kwa ujumla.Pia kuna baadhi ya kampuni yaliyohusika pia kwenye matayarisho ya sheshe hii ikiwemo RADIO JAHAZI ,DENTAL ART CENTRE na,IFLY, BONEFIRE ADVENTURES.Kampuni hizi tumezifatilia tuwaulizie kuhusu kama wanajua chochote kuhusiana na malipo lakini nyingi wamedai hawana uhusiano na mambo ya malipo sababu hao walisaidia maandalizi tu.Kuna tetesi kuwa huenda leo wakalipwa but tunahakikisha ukweli huo isiwe ni propaganda.Tunafikiria hii kuanika mitandaoni ndiyo imepelekea kulipwa wanachotarajia wasanii leo.#Fuatilia stori hii kwa blog yetu.#MADEINMALINDI..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment