Imebainika kwamba ngoma inayozidi kupata sapoti ya nguvu kwenye mitandao,radio na hata vituo vya runinga kote nchini,GONGA PIA ya Fash P mwanzoni ilianza kama project ya Fash P akiwa amemshirikisha mwamba wa masauti ndani ya County 003 ,Jaslu. Project hii inavyosemekana ilianza chini ya Producer Big Zoo ambaye ndiye mwanzilishi wa biti na Fash P kufanya ngoma hiyo akiwa pekee na baadaye kuondoka na data ya ngoma hiyo.Kilichofuata ni kwamba Fash P alimtafuta Jaslu na wakakutana ndani ya himaya ya Producer mkongwe mjini Malindi ,Jokka Zunda.
Kama tulivyozipokea habari hizi ni kwamba project ile ikafunguliwa pale na Jaslu akaweka chorus ya ngoma hiyo.Data iliyotoka kwa Jokka Zunda ilipelekwa Crack Sound ili Kufanyiwa mastering. Hapo ndipo mambo yalipogeuka na chorus ya Jaslu kutolewa, beat ya Big Zoo kubomolewa na Producer Dhilly na nafasi ya Jaslu ikajazwa na CRASH V! Inavyosemekana Jaslu hakuridhishwa na hilo na huenda ikawa uhusiano kati ya wawili hao sio sawa.Haijabainika nini kilichopelekea Fash P kufanya uamuzi huo lakini bado tunazifuatilia habari hizi.Pakua ngoma zote mbili halafu usikose kutoa maoni yako hapo kwenye comment box kama kali ni ipi.
No comments:
Post a Comment