Wednesday, 5 June 2019

FASH P KUISAMBARATISHA GMBA LORDS MUSIC #GLM


Msanii wa Rap kutoka County 003 kanda ya Pwani ya Kenya, Fash P ,ambaye pia ni kiongozi wa Label ya GLM ( Gmba Lords Music ) ameonekana kufanya kazi na kujihusisha na wasanii wengine mbali na wasanii wenza kutoka Label hiyo.Huu mwaka Fash aliuingia na Project inayojulikana kama GONGA PIA  aliyomshirikisha CRASH V ambayo bado inaendelea kupokelewa vyema na mafans wake kote nchini.

GONGA PIA ni project ambayo imemletea mafanikio msanii huyo baada ya video ya ngoma hiyo kupata sapoti kubwa kwenye vituo vya runinga humu nchini vikiwemo Citizen TV ,Focus TV na KTN.Kuna kazi mpya itakayodondoka wakati wowote kuanzia sasa kutoka kwa msanii huyo.Tulipomhoji ,Fash P ilifunguka na kuweka wazi kuwa ujio huo pia hakuhusisha msanii yeyote kutoka Gmba Lords Music.Alitupa fununu tu ya kuwa msanii aliyeshirikiana naye kwenye kazi mpya ni msanii ambaye wakati wa nyuma aliwahi kufanya naye kazi.Je,ni kweli kikundi na lable hiyo ilisambaratika? na Je, msanii huyo aliyeshirikishwa na Fash kwenye kazi yake mpya ni nani? Usikose kutembelea blog yetu kwa habari zaidi.Subscribe kwa channel ya Fash P HAPA

No comments:

Post a Comment