Friday, 31 May 2019
UJIO MPYA WA KIDDOH KATULUNGE
Msanii mpya anatangaza ujio wake kwenye ulingo .Hii imejitokeza leo Nuktasaba ilipogongana na msanii huyo ndani ya MALINDI CITY A.K.A CHOCOLATE CITY.Msanii huyu ameongea mengi na Nuktasaba kama ifuatavyo:-
"Mimi ni msanii mpya wa kizazi kipya.Kwa jina naitwa KIDDOH KATULUNGE .Nmeanza muziki mwanzo wa 2019.Ninafanya kazi studio inayoitwa SOLID RECORDS iliyoko mtaa wa MUYEYE ,MALINDI CITY chini ya produsa KIWANJA.Nyimbo ya kwanza ninayotaka kuiachilia inaitwa TOTOTOH.Nyimbo hiyo iliyoko tayari kwa sasa inaongelea mrembo flani ninayepanga kumdeti soon.Track hii naeleza kumhusu vile vigezo ninavyotaka awe navyo ndio nimpende.Hiyo ndio sababu nimetumia neno la kimijikenda awe TOTOTOH yaani awe vizuri na muonekano kabambe apendeze hata mafisi wamtamani.Nyimbo hii naaminia itapokelewa vizuri na mafans wakiisikia sababu produsa KIWANJA ametulia kwenye beat nami nimenata na hisia kali.Mafans nawaomba ifikapo tarehe 8/6/2019 nikiachilia kichupa hicho mnipe sapoti kali.Nawaahidi sitawaangusha sababu hata video ya ngoma hii iko kwenye mpangilio si kitambo mtaipata pia.Kazi zangu nitazieka kwa mitandao na mafans wangu mtazipata kwa urahisi .Mwisho nawaambia msiwe mbali tegeeni tu TOTOTOH ikidondoka mtaipata mitandaoni so be ready kwa ujio wangu mpya,I LOVE YOU ALL ".
Hivyo ndo msanii huyo alivyofunguka na kazi hiyo akiidondosha utaipata hapa Nuktasaba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Na support Nazi ako kea sanaa tu...ache tungojee tootooh ra kimidzichenda...likiangushwa
ReplyDelete