Saturday, 18 May 2019

TUNALIAMSHA JUMATATU!


Mwanadada anayekwenda kwa jina la kazi kama Sister Shanniez ,ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio Kaya kwa kipindi kirefu ,sasa anarudi hewani rasmi kuanzia Jumatatu wiki ijayo tarehe 20.Anti Virus kama wengi wanavyomfahamu kutokana na jukumu alilonalo katika tasnia ya mziki kama mshika dau,amedhihirisha kuwa atakuwa akiendesha kipindi cha Take Over kupitia Msenangu F.M.


Kupitia mtandao wake wa Twitter, Shanniez ameweka wazi kuwa atakuwa anatake over kupitia 99.5 Mombasa ,92.5 Mld kuanzia saa nne mpaka saa saba mchana.Amewaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti kwa kuskiza na kuchangia kwenye kipindi hicho kupitia hashtag #TakeOver995 .Msenangu F.M, Haha Ni Hehu!

No comments:

Post a Comment