Wednesday, 22 May 2019
CHUNAA KARUDI.MPANGO WA KANDO KAFELI .!
Hatima ya mpango wa kando ulifeli juzi wakati mama mwenye boma aliporudi toka majuu.Video vixen huyo anayeitwa CYNTHIA JHENE
aliyekuwa akimnyemelea msanii SWANYO BOY itabidi akae benchi kwa sasa sababu mrembo wa SWANYO BOY anayeitwa FARHIYA ROTICH kazama mjengo tena kutoka ughaibuni alikokwenda kikazi miaka minne iliyopita
.Kwa sasa SWANYO BOY hana tena ujanja.Hata yambidi akae chini na mrembo wake mwenye asili ya Ki.Ethiopia wapange kazi kwani chimama huyo ndiye aliyemlipia gharama za studio za nyimbo alizofanya kama tulivyopata habari baada ya kumhoji staa huyo anayekuja kwa kasi sana kwenye sanaa.SWANYO BOY ameongea hivi " Mrembo huyu tumetoana mbali sana yaani niliishi naye miaka mitano kabla ya kupata safari yake ya ng'ambo.Alinisaidia kwenye muziki wangu hata kunilipia gharama za studio ya nyimbo zangu mbili.Hata ile track ya CHUNA ilikuwa ni dedication yake yaani nilikuwa namuimba yeye.
Kwa sasa anataka anilipie track ingine mpya nifanye na video kwa pamoja.Pia nina mpango wa kufunga ndoa naye ifikapo mwaka ujao so kwa sasa nko booked yaani nko fully na mama mwenye nyumba ndani." Msanii huyu alionyesha uamuzi wake wa kiutu uzima kumaanisha yuko serious raundi hii.Lakini swali ni ,Je ataweza kuweka uaminifu sababu vyenye anaendelea kupata umaarufu ndivyo warembo wa nje wanazidi kumtamani ? Tusuburi tuone ..!
Kwa sasa SWANYO BOY anagonga vichwa na BOUNTY KILLER inayofanya vizuri kwa mitandao na chati za pwani lakini mashabiki wanangoja hicho kibao kipya msanii huyo aliahidi kama kitakuwa hit pia.Tusubirie tu kikiachiliwa tunakudondoshea hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment