Wednesday, 17 April 2019

SWANYOBOY AZIDI KUKINUKISHA..!

Msanii anayepeta kutoka MK2 STUDIO kwa jina SWANYOBOY akinukisha tena.Mkali huyo aliyepost picha mitandaoni na msanii hatari anayefahamika kama MAMA LAO hivi majuzi ikadaiwa ashamposa MAMA LAO na kwa sasa anaendelea kuvuma na mpini uitwao BOUNTY KILLER.Alipohojiwa na meza yetu amedai "Raundi hii nataka nitawale kimuziki apa nchini Kenya na East Africa yote kwa jumla ndo saa hii nawachapa mafans na track ya BOUNTY KILLER".Ameongeza kuwa nyimbo hiyo si kitambo ataachilia video yake na kazi hiyo itafanywa na video produsa kutoka Tanzania ambaye kwa sasa wanaendelea kufunga dili hiyo.Kwa kweli SWANYOBOY ana uwezo mkubwa sana kwa jinsi anavyotetemesha radio za pwani na Kenya kwa sasa.Msanii huyu huenda mwaka huu akafaulu sana kimuziki ata maybe mwaka huu anaweza miliki mkoko wake binafsi kama alivyotudokezea kwenye mazungumzo fulani siku za nyuma na meza yetu.Ukitaka kuisikiza ngoma hiyo ipate http://mdundo.com/song/1304721?appshare.Kwa kweli tunamutakia kila la heri kwenye safari yake ya muziki.

1 comment: