Sunday, 21 April 2019

KWANINI SIKUPANDA JUKWAANI HUKO MALINDI

Mbosso amedhihirisha kukerwa na waliohusika katika kupanga na kuandaa tamasha lililojulikana kama Malindi Festival.Tamasha hili lilikuwa limepangwa kufanyika Ocean Beach Resort & SPA mjini Malindi jumamosi tarehe 20 mwezi wa nne.Msanii huyo wa WCB ameweka wazi kupitia mtandao wake wa Instagram  kuwa mipangilio ya tamasha hilo haikuenda kulingana na mkataba. Management ya Mbosso ndiyo iliyositisha kupanda kwake jukwaani.Tumejaribu kuwatafuta waandalizi wa tamasha hilo ila harakati zetu bado hazijafua dafu.Sanaa ni kazi kama kazi nyengine na kulingana na mtazamo wa NUKTASABA ,waandaaji wa matamasha kama haya wajukumike!

No comments:

Post a Comment