Tuesday, 23 April 2019
HALI SIO SHWARI
Fash P ni miongoni mwa wasanii wa Hip Hop kutoka Pwani ya Kenya hususan Malindi.Hivi majuzi,kupitia ukurasa wake wa Facebook , alionekana kuwa katika harakati za kufanya kazi yake mpya na tulitaka kama NUKTASABA kujua kama kazi hii imefikia wapi."Nimerekodi tayari ,bado tu mambo kidogo tuachie ngoma.Nimeshirikiana na msanii flani wa Kilifi kwenye chorus ambaye pia anaweza.Tulikuwa tumepanga tutoe ngoma hiyo pamoja na video yake mwezi huu wa nne lakini hali upande wangu sio shwari kwa sasa.Nilihusika kwenye ajali ambayo imepelekea kuniumiza mguu wangu wa kushoto.Kulingana na Daktari, nimepewa mpaka mwezi wa tano ndio niweze kurudia shughuli zangu za kawaida.Kwa mafans wangu,waendelee kusupport GONGA PIA - FASH P FT CRASH V wakisubiri kazi hiyo mpya",alitueleza msanii huyo. Tunamuombea Fash P afueni ya haraka ili aweze kutekeleza mipango yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment