Tuesday, 28 January 2020

HAIJAPOKELEWA VIZURI NA MASHABIKI#RADIO JAHAZI

Msanii kutoka Chocolate City yaani MALINDI anayefahamika kama NELLY BOY kaachilia kazi mpya kwa Jina CHUKI.Kwa kweli nyimbo hii haijapokelewa vyema na mashabiki wake wa Radio JAHAZI 87.7 ~MALINDI. Wanadai kwamba mwana alibana sauti sana.. Wengine wanalalamika ni kama ambaye aliimba akiwa bafu na kaishiwa na pumzi . Malalamishi mengine yameongezeka kwamba ni kama alikuwa hana mood ya kuimba wakati akifanya hii kazi. Pia kuna tetesi  zadai hajabadilisha idea, bado ni ile ile ya kutemwa na mademu.Mafans wamemalizia kumshauri abadilishe idea waendelee kumpa support ama wamuachilie.! Tunamtafuta NELLY  BOY atupe ukweli juu ya swala hili na kama ni kweli basi arekebishe makosa yake ili aendelee kupokea support tokea kwa mafans wa Radio JAHAZI 87.7 Fm ~Malindi.Asipochange basi mafans wamteme tu.

6 comments:

  1. Duh.. Hata hivyo idea ni moja tu

    ReplyDelete
  2. Huyu dogo anajitahidi Sana,ila mafans wa radio jahazi wamezoea nyimbo za wasafi ju mapresenters wote hizo ndo nyimbo zao, they don't want to support Malindi music

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umebonga point.
      Let's support Malindi artist lakini kama ni kushabikia wasanii wa studio Fulani then mziki utaishia hapa hapa Malindi.

      Delete
    2. Kuna ukweli hapa#Let's support Malindi Music but Kama unakosolewa NELLY BOY rekebisha makosa yako coz mashabiki wako ndio maboss wako#

      Delete
  3. Nelly boy ni msanii anayejituma sana hapa Malindi hivyo basi uimbaji wa tracks zake kutumia visa tendwa isiwe kigezo cha mapresenter kubagua ngoma zake Kwani kwenye hii Sana ya mziki yeye sio msanii wa kwanza kutunga ngoma kulingana na visa vya kutendwaaa na kulalamikia kutemwa.
    Kuna wasanii kadhaa ambao tumeona wakililia na kulalamikia kutendwaaa na kupitia idea hizi ndo zimewatoa.
    Endapo kama wewe ni shabiki au hata presenter na unafuatilia sana hii industry then lazima umeona Diamond platinumz msanii wa Tanzania akiimba visa sawia vya kutemwa na kutendwaaa na watoto wa kike.
    Nmeamua kuwapa mfano ulio hai ambao umemtoa Diamond platinums.
    Kwa mfano ngoma hizi zilitinguka kulingana visa vya kutemwa na kutendwaaa.
    1.NALIA NA MENGI:Hapa Diamond Amalia kisa katendwaaa.
    2.MOYO WANGU:Diamond analaumu na kulilia kutendwaaa huku akilaumu moyo mbona amependa na mwisho kutendwaaa.
    3.NATAKA KULEWA:Ni wazi hapa Diamond analitendwa na anataka kulewa angalau ajifariji.
    4.MAWAZO:Hii ngoma aliimba Diamond kisa katemwaa hivyo basi akaamua kutunga akieleza hisia zake after kutemwaa.
    5.NIMPENDE NANI:Diamond baada ya kutendwaaa akasema ampende nani coz alikuwa keshazenguliwa na mtoto wa kikee.
    *****************
    Hapa Diamond aliimba ngoma mingi sana akilalamikia kutemwa nakutendwaaa.
    Kuna wasanii kibao wamelalamika kutendwaaa..
    1.Sagna-Sitaki kuumizwa
    2.Best Naso:Narudi kijijini
    3.PNC:Baby mbona
    4.Abby skillz:Ngo!ngo!ngo
    5.Lavalava-Gundu/Bora tuachane.
    *************
    Kuna wasanii wameimba kuhusu idea ya siasa na kutoa zaidi ya ngoma 5 kwa idea moja.
    >>>>>SUSUMILA ni mfano hai...
    1.SIASA DUNI
    2.KILA MTU
    3.HAKI
    .......N.K..
    ************
    Hivyo basi Nelly boy sio wa kwanza kuimba ngoma kulingana na idea moja.
    Kila msanii anaujio tofauti style yake kuimba so mghala muueni Haki yake mmpe.
    **********
    Kuhusu sauti atarekebishaa Ila mimi naona haina shida coz kama ulisikiza sauti ya mwimbaji Jose Chameleone wa Uganda then hapa utakuwa umepata jibu.

    ReplyDelete