Friday, 25 October 2019

HAKUNA MAFANIKIO BILA UPENDO .!

Kweli jambo hili limeregesha nyuma sanaa ukanda wa pwani na Kenya kwa ujumla.Hii imedhihirika kwenye sanaa kuwa hakuna upendo katika  sekta ya muziki na hili ndilo limechelewesha mafanikio mpaka sasa hivi kwa wasanii wetu yaani wasanii waliofaulu kimuziki ni kidogo sana.Kwa mfano hapa pwani kuna wasanii wengi zaidi za maelfu lakini wanaojulikana ni baadhi na hao baadhi hawataki kuchukua hatua kusonga mbele kimaisha na kibiashara.Utashangaa msanii alianza mziki 2000 lakini hana msingi wala biashara yoyote .Kazi ni kupata mashow na kupiga sheshe na kujionyesha .Si wasanii wetu tungeiga mfano wa wenzetu wa Bongo kama vile JUX ana cloth line yake na anauza vizuri, Mwengine ni MR BLUE pia ana bonge la boutique iliyoimarika. 

Pia hapa county 003  tupo nao kidogo wanaojaribu kujimudu kibiashara kama LANGE MWEPESI anayemiliki lebo ya GALLANT PERFUMES.

Lakini ni wasanii kidogo wengine wanaomiliki biashara zao.Hii  inasababishwa na ukosefu wa upendo.Unakuta wasanii wanatengana,hali ya kuwa hawajengani.Kwa mfano siku hizi kuna mitandao kama yutube na whatsap ambapo wasanii huachilia kazi zao .Cha kushangaza utaona msanii ameachilia kazi yake halafu inapata views 30 baada ya miezi miwili ilihali ya kazi ya msanii wa Bongo ama Naija inapata views mamillioni baada ya wiki moja.Kitu hiki kinaonyesha hakuna upendo.Jambo hili linaumiza sana  sanaa.Kumekuwa pia na tetesi kwamba wasanii wengine wanapendelewa na maredio fulani kuliko wengine.Jambo hili linafelisha mafanikio.Pia kuna studio zengine zinapendelea wasanii kadhaa zaidi kuliko wengine.Si Jambo hili linagandamiza sanaa ya Kenya.Si wasanii na mashabiki wote wangekuwa na upendo si wasanii wangefika mbali.Ama hatujajiuliza ni wapi tunafeli ? Haipendezi msanii Kama RAYVANNY atoke bongo aje Kenya achukue mamilioni Kenya ilihali msanii wetu akieka show watu hawaendi.Hii inaonyesha hakuna upendo.Na bila upendo wasanii hawatafanikiwa. Inastahili wakenya tulete upendo kwenye sanaa ndiyo mafanikio yatakuja.Tukieneza upendo sanaa itafika mbali.Hatuoni mfano kama wa HARMONIZE alivyomregesha Q CHILLAH kwenye game aliyekuwa amepotea.Hii ni upendo.Hapa Kenya si kuna mastaa waliopotea kama vile SOKORO,BAD MASTERS,PHARAOH,SIR OWI ,KENNOH G,CZARS,RANNY na wengine mob ambao wangepata  support kwa wasanii waliofanikiwa si muziki ungeenda mbali.Hii ni baadhi ya mifano lakini cha muhimu ni wasanii na mashabiki tuwe na upendo ndiyo kutakuwa na mafanikio.Tukiwa na upendo wasanii watafanikiwa ,haitakuwa ajabu msanii atoe nyimbo mbili na awe na uwezo wa kumiliki mkoko.Itawezekana tukiwa na upendo.

4 comments: