Friday, 26 July 2019

NGOMA NI YANGU SIO YA FASH P!


Msanii mkongwe wa mziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mmiliki wa studio za Pillar Works Malindi ,Kleanheart ,adai kuwa ngoma ya Sina Sababu iliyofanywa na Fash P ,Mchafuzy pamoja na yeye ni utunzi wake.Alipokuwa katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Jahazi 87.7 Malindi akiwa na The Captain kwenye kipindi cha Mzuka Levo, Fash P kwa upande wake alifunguka na kudai kwamba kufikia wakati anakwenda hewani,ngoma hiyo ni yake.Fash P pia vilevile aliutambua mchango wa Kleanheart kwenye kazi hiyo inayokwenda kwa jina Sina Sababu.Ilivyobainika kutokana na mahojiano hayo ni kwamba chanzo cha ngoma hiyo kilianza kwa Kleanheart,tukizungumzia beat na chorus.


Baada ya kufanya  chorus Kleanheart inasemekana alimtafuta Fash P na kumpa kazi hiyo ili aandike na kurekodi vesi zote tatu na ngoma hiyo iwe yake jambo ambalo Fash alilifanya kwa kushirikiana na Zere Lao, Mchafuzi.Video ya ngoma hiyo ilipotoka ,Kleanheart aliiweka kwa channel yake ya YouTube lakini haikupita muda mrefu Kleanheart alitumiwa jumbe mitandaoni kwamba Sina Sababu sio kazi yake na shirika linalosemekana Fash P aliweka mikataba nalo ili kumtunzia hakimiliki za kazi zake.Baadaye shirika hilo liliiondoa video ya Sina Sababu kwenye Channel ya Kleanheart jambo ambalo Kleanheart hakuchukulia poa.Je,nani anafaa kuwa mmiliki halali wa ngoma hiyo?


No comments:

Post a Comment