Monday, 30 April 2018
MSANII WA SIKU
Leo tuko na msanii mkali wa siku anayefahamika kwa jina BIG ZOO kama tunavyojulishwa na ripota wa kitengo hicho.BIG ZOO ni PRODUSA aliyefanya na industry kwa miaka kumi sasa.Aliingia kwenye industry mwaka wa 2008 na studio kwa jina ZOO RECORDS.Alifanya kwa muda lakini kwa sababu alitaka kuwa maarufu ikabidi atafute studio nyingine ili azidi kukomaza kipaji chake.Alijiunga na V.I.P RECORDS hapa KijiweTanga.Alizidi kukua kikazi akaanza kuwa mashuhuri.Sifa izi zake zikamfanya apate deal safi na Studio ingine ..Studio hiyo iliitwa TRUE KRAZY RECORDS iliyoko mtaa wa Kisumu Ndogo Malindi.Katika Studio hii amefanya kazi na wasanii wakubwa ikiwemo J.I ,SHABBIG,BROWN BOY,MADOLA na wengineo.Produsa huyu amekuwa mkali sana kwa kazi zake na ameweza kufanya wasanii kujulikana ikiwemo MWANGAZA FAMILY na kibao MGANGA,LUCKY BOY -MAUMIVU, EMANIZO kibao PESA na STIM KICHWAN ngoma THABIA KOLO inayopenda sana kuchezwa na watangazaji wa Pwani FM na stesheni zingine hapa Kenya.Mwaka huu mwanzo alihamia studio ya 254 CLASSIC STUDIO anakofanyia kazi mpaka saa hii.Produsa huyu ana ustadi sana kwenye kazi zake kitu kinachomfanya kudondosha ngoma zinazobamba mafans wazisikiapo.Ndoto ya BIG ZOO ni kuwa Produsa mkali nchini Kenya na huenda hii ikatimia sababu ana bidii na ni mwingi wa ubunifu kwenye mabeat ..Alipoulizwa na ripota wetu kuhusu changamoto za kazi yake amedai wasanii wengi awapatao huwa wako chini kimaisha ,mara nyingi huwa hawana mtaji wa kulipa studio so hubidi kuwatengezea kazi na kuwalea kwenye sana mpaka wajulikane.Kwa kweli BIG ZOO humbidi atafute mapromota ambao watamsaidia kuinua hii sanaa.Alipoulizwa kuhusu mbinu ya kusaidia kuinua wasanii wake alijibu kwa sasa ameeka nyimbo za wasanii wake kwenye mitandao jambo linalosaidia kujulikana kwao na kujenga majina yao.Jambo hili liligusa sana team NuktaSaba na waliapa watamsaidia kuinua kazi zake kwenye mitandao.Mwisho akatoa huu ujumbe kwa mafans wake "MTOTO HAKUI KWA BABAKE,MTOTO NI MTOTO TU SO WASANII WASIKIZAO MAPRODUSA WAO HUTOBOA NA KUFIKA MBALI".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment